Saturday, February 9, 2013

MADIWANI TUNDURU WAPITISHA BAJETI YAO


Na Steven Augustino,
Tunduru.

BARAZA la madiwani wa hlamashauri ya wilaya ya Tunduru Ruvuma limepitisha rasimu ya mpango wa bajeti ya matarajio ya kukusanya na kutumia kiasio cha shilingi bilioni 34,425,566,350 katika kipindi cha mwaka  2013hadi 2014.

Akiwasilisha hivi karibuni taarifa hiyo kwa niaba ya Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya hiyo Robert Nehatta katika kikao hicho kilicho fanyika ukumbi wa Klasta mjini hapa, afisa mipango wa wilaya hiyo Keneth Haule alisema kuwa kiasi hicho ni sawa na ongezeko la shilingi bilioni 6,881,058,813 sawa na asilimia 19.9% ikilinganishwa na bajeti ya shilingi. bilioni 27,544,507,537 zilizo idhinishwa katika bajeti ya mwaka 2012 hadi 2013.

Akifafanua taarifa hiyo Bw. Haule alisema kuwa katika ya fedha hizo Shilingi 34,425,566,350 zitatokana na makosanyo ya ndani vya halmashauri hiyo,Ruzuku ya matumizi ya kawaida tsh.18,174,302,120 Mishahara shilingi 18,868,732,200 na matumizi mengineyo (PE) ni Tsh.2,237,201,000.


Taarifa hiyo iliyodaiwa huhitaji baraka za waheshimiwa Madiwani wa wilaya ya Tunduru baada ya kupitiwa na kamati husika iliendelea kufafanua kuwa kiasi cha shilingi 10,386,289,944 kitatokana na fedha za ruzuku ya fedha za miradi ya maendeleo, pamoja na shilingi 310,716,000 fedha kutoka katika mfuko wa kufidia vyanzo vya mapato vilivyofutwa (GPG).  

Haule aliendelea kufafanua kuwa kati ya fedha hizo halmashauri hiyo inatarajia kutumia shilingi 34,425,566,350 ambapo kati ya fedha hizo shilingi  21,105,933,200 zimepangwa kutumika katika matumizi ya kawaida.

Taarifa hiyo iliendelea kueleza kuwa kitengo cha mishahara kwa watumishi zimepangwa shilingi 18,868,732,200 na kifungu cha matumizi mengineyo kimepangiwa shilingi 2,237,201,000 huku miradi ya maendeleo ikipangiwa shilingi 10,386,289,944.

Awali akifumgua na kufunga kikao hicho maalumu cha baraza hilo Mwenyekitri wa halmashauri ya wilaya hiyo Faridu Khamisi, aliwataka madiwani hao kutoa ushirikiano kwa watendaji, ili kuwezesha halmashauri yao kupiga hatua za maendeleo.         

No comments: