Thursday, April 11, 2013

BREAKING NEWS: MWANDISHI NA OFISA UHAMIAJI WAFARIKI DUNIA KATIKA AJALI YA GARI, WENGINE WAJERUHIWA VIBAYA



Na Mwandishi wetu,
Tanga.

WATU wawili wamefariki dunia na wengine wanne kujeruhiwa vibaya hivi punde, baada ya kutokea ajali katika wilaya ya Handeni wilayani Tanga.

Waliofariki dunia ni Mwandishi wa habari wa Uhuru na Mzalendo na Radio Aboud, Hamis Bwanga na Ofisa uhamiaji wa wilaya ya Handeni, Mariam Hassan akiwemo pia Mwandishi wa gazeti la Mwananchi Hussein Semdoe ambaye amejeruhiwa vibaya na hali yake sio nzuri mpaka sasa.


Ajali hiyo imetokea muda mfupi uliopita, baada ya tairi la gari walilopanda aina ya Nissan, kupasuka na kusababisha gari hilo kupinduka.

Majeruhi wamepelekwa katika hospitali ya wilaya ya Handeni na kwamba ajali hiyo imetokea katika kijiji cha Misima, kilichopo wilayani humo.

Mkuu wa wilaya ya Handeni, Muhingo Rwehemamu amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.

Naye Kamanda wa polisi wa mkoa wa Tanga Costantine Massawe amesema, hivi sasa taarifa kuhusu ajali hiyo inaandaliwa ambapo ikishakamilika itatolewa baadaye, kwa vyombo mbalimbali vya habari.

No comments: