Wednesday, April 3, 2013

TUNDURU WALIA NA HALI NGUMU YA MAISHA, KUTOKANA NA WAJANJA WACHACHE KUJINUFAISHA KATIKA ZAO LA KOROSHO



Na Steven Augustino,

Tunduru.


CHAMA cha Wananchi CUF Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma, kimewaomba wananchi wa wilaya hiyo kutotoa nafasi kwa viongozi watakaosimamishwa kugombea nafasi mbalimbali za uongozi katika chaguzi zijazo.

Hayo yalibainishwa na Viongozi wa chama hicho wakati wakizungumza katika mkutano wa hadhara, uliofanyika katika viwanja vya baraza la Idd na kuongeza kuwa kauli hiyo wanaitoa kufuatia viongozi wa CCM waliopewa dhamana na wananchi kushindwa kutimiza wajibu wao.

Mkurugenzi wa haki za bianadamu na sheria  Mtukumbe Selemen Issa Ismail na Katibu wa CUF wilaya  Mchemela Salum Abudalah  ni miongoni mwa waliobainisha maelezo hayo, na kuongeza kuwa hali hiyo inatokana na viongozi waliopewa mamlaka hayo kutotimiza wajibu wao na kusababisha hata zao la Korosho wilayani humo, wakulima kukosa soko la uhakika.


Walisema kutokana na hali hiyo hivi sasa wananchi wa wilaya hiyo wanaishi maisha ya kukata tama, hali ambayo imewafanya washindwe hata kupeleka watoto wao shule huku huduma ya chakula majumbani mwao, ikiwa ni shida.

Aidha katika hotuba hiyo pia viongozi hao wakagusia makali ya maisha katika upatikanaji wa huduma za afya, kupanda kwa bidha ambako walidai kuwa ni kikwazo kikubwa katika maendeleo ya wananchi wa wilaya hiyo.

Akihutubia kwa staili ya kulia huku akibubujikwa na machozi mjumbe wa kamati ya siasa CUF wilaya ya Tunduru  Said Kiosa alisema kuwa kinacho waponza na kuwafanya wapatwe na madhila hayo, Wanatunduru ni tabia zao za upole na kuridhika na kila linaloelezwa kuwa ni zuri kwao.

Kufuatia hali hiyo aliwataka wananchi hao kubadilika na kutetea maendeleo yao, na ikishindikana iwe hata kwa kumwaga damu kama walivyofanya wenzao wa wilaya za Masasi, Tandahima na Mtwara vinginevyo wataendelea kubaki nyuma, huku mali zao zinaporwa na kuwanufaisha wajanja wachache. 


No comments: