Tuesday, April 30, 2013

WANAFUNZI WAFARIKI DUNIA KWENYE DIMBWI LA MAJI

Na Mwandishi wetu,
Tarime.

WANAFUNZI wawili wanaosoma darasa la sita wilayani Tarime, wamekutwa na mauti baada ya kuzama katika dimbwi lenye tope na maji mengi.

Wanafunzi hao ni wa shule ya msingi Nyamwaga, katika kijiji cha Nyakunguru, kata ya Kibasuka wilayani humo.


Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na kamanda wa polisi kanda maalum Tarime/Rorya, Justus Kamugisha aliwataja  wanafunzi hao kuwa ni  Richard Mniko (16) na Mniko Melengali (16).

Alisema wanafunzi hao wote wawili walizama katika dimbwi hilo, baada ya kutumbukia kwa madhumuni ya kutaka kuogelea.

Wanafunzi hao walitumbukia katika dumbwi
hilo Aprili 28 mwaka huu majira ya mchana, lakini walishindwa kuogelea kutokana na tope na maji kuwa mengi.

No comments: