Tuesday, April 9, 2013

UHURU AAPISHWA KUWA RAIS WA KENYA, AHUTUBIA TAIFA

Kulia ni Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta na Makamu wa Rais wa nchi hiyo Wiliiam Ruto baada ya kuapishwa hivi punde.



















UHURU Kenyatta ameapishwa kuwa rais mpya wa Kenya akifuatiwa na William Ruto ambaye hivi punde ameapishwa naye kuwa Makamu wa Rais wa Kenya.

Msajili wa Mahakama, Gladys Shollei ndio amemuapisha Uhuru Kenyatta kuwa rais wa nne Kenya na baadaye amemuapisha William Ruto kuwa Makamu wa Rais wan chi hiyo.

Marais mbalimbali wamewasili  hivi punde katika Uwanja wa Karasani kwa ajili ya kushudia kuapishwa kwa rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta.


Miongoni mwa marais walioudhuria sherehe za kuapishwa kwa Uhuru Kenyatta ni rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe, Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania, Rais Yoweri Museveni wa Uganda, na Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini.

Wengine ni Salva Kiir Mayardit wa Sudani Kusini, Rais Paul Kagame wa Rwanda. Wengine ni Jaji Mkuu wa Mahakama ya Juu ya Kenya, Willy Mutunga, Msajili wa Mahakama, Gladys Shollei Makamu wa Rais wa Kenya, William Ruto, na mama yake Uhuru ambaye ni mama Ngina Kenyatta. Pia mke wa Uhuru Kenyatta amekuwa miongoni mwa wageni waalikuwa.

Pia bila kumsahau Rais Mwai Kibaki anayemaliza muda wake naye ameshudia kuapishwa kwa Uhuru Kenyatta ambaye muda mchache ujao utamkabidhi madaraka ya Urais.

Pia hivi punde habarimasai.com imeshuhudia Rais Uhuru Kenyatta akikabidhiwa Katiba pamoja na mambo mengine.


Kivutio kikubwa katika sherehe hizo ni Uhuru Kenyatta ambaye ameusisimua uwanja wa Karasani ambao umefurika watu wengi wakati akiingia na wakati akitia saini kwa mkono wake wa kushoto.

Hivi sasa Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta anakilihutubia Taifa kwa mara ya kwanza tangu alipochaguliwa kuwa rais wa nne wa nchi hiyo.

No comments: