Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu. |
SERIKALI imetangaza kuwachunguza waganga na wauguzi,
wanaomiliki hospitali, kliniki na maduka ya dawa baridi ili kubaini kama
wanahusika na upotevu wa dawa kwenye hospitali za Serikali.
Akizungumza ofisini kwake jana, Waziri wa Afya Ummy Mwalimu
alisema Desemba 26 alipotembelea Hospitali ya Ocean Road, aliamua kuunda kamati
ya watu watano kuchunguza kama wanahusika na upotevu wa dawa hospitalini hapo
na sehemu nyingine.
Alisema bodi ya hospitali hiyo aliyoiunda wiki mbili
zilizopita, nayo imeshaanza kufanya kazi ya kubaini chanzo cha uhaba wa dawa
hospitalini hapo.
“Hata ukisoma tamko langu, hatukatazi watumishi wa umma wa
sekta ya afya kumiliki hospitali, kliniki au maduka ya dawa, lakini tunachoangalia
ni namna gani tunaondoa mgongano wa kimasilahi,” alisema.
“Nimeenda Ocean Road, wagonjwa wanakufa kwa kukosa dawa,
tusubiri kamati itoe taarifa.”
Alisema katika ziara yake aligundua madudu mengi ikiwamo pia
fedha za bajeti ya dawa zilizokuwa zikipangwa kwa ajili ya hospitali hiyo,
kutofika kwa wakati zilizokuwa zikipangwa kwa ajili ya hospitali hiyo, kutofika
kwa wakati.
Waziri Mwalimu alisema asilimia kubwa ya wagonjwa wanaotibiwa
hospitalini hapo ni maskini,na kwamba watu wenye uwezo hutibiwa katika
hospitali kubwa za kulipia na wengine wanatumia bima ya afya.
“Kwa kuwanyima dawa wanaokuja hospitali hizi ni sawa na
kuwanyanyasa,” alisema Waziri Mwalimu.
“Bajeti ya dawa inayopangiwa hospitali hiyo imeonekana nyingi
zilikuwa hazifiki kwa wakati. Nimeshamuagiza katibu mkuu wa wizara yangu
ahakiki kila fedha zinazopelekwa kwa ajili ya kununua dawa wizarani.”
No comments:
Post a Comment