TUNAPOELEKEA
kumaliza mwaka huu 2015 na kuukaribisha mwaka mpya wa 2016,
wananchi hutumia muda huo kwenda katika nyumba za ibada ama kusherekea
katika maeneo mbalimbali ya starehe, ambapo uzoefu unaonyesha kuwa baadhi ya
watu hupenda kutumia fursa hiyo kufanya vitendo vinavyohatarisha usalama
wa raia mali zao.
Jeshi
la Polisi nchini, limejipanga vizuri katika mikoa yote kwa kushirikiana na
vyombo vingine vya ulinzi na usalama ili kuhakikisha kwamba vitendo vyovyote
vya uhalifu vitakavyojitokeza hususan katika kipindi hiki cha kuelekea
mkesha wa mwaka mpya vinadhibitiwa.
Ulinzi
umeimarishwa kwenye maeneo yote ya ibada, fukwe za bahari, sehemu za starehe na
maeneo mengine yote ambayo yatakuwa na mikusanyiko mikubwa ya watu.
Aidha, Jeshi
la Polisi linatoa tahadhari kwa wananchi wote kuwa makini na kuchukua hatua
stahiki za haraka kwa kutoa taarifa pindi wanapoona viashiria vyovyote vya
uhalifu katika maeneo yao ya makazi ama maeneo ya biashara. Simu za polisi
endapo mwananchi atakuwa na taarifa ni 111 au 112.
Pia
Jeshi la Polisi linawatahadharisha wale wote, ambao watakuwa wakitumia barabara
kuwa makini na kuzingatia sheria za usalama barabarani na hasa kwa madereva wa
magari na pikipiki, kuepuka kujaza watu kupita kiasi, kwenda mwendo kasi,
kutumia vilevi pamoja na kupiga honi hovyo.
Vilevile,
wananchi kuacha tabia ya kuchoma matairi barabani pamoja na kupiga mafataki.
Aidha yeyote atakayefanya vitendo hivyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa
dhidi yake.
Nawatakieni
watanzania wote kheri ya mwaka mpya.
Imetolewa
na:
Advera
John Bulimba-SSP
Msemaji
wa Jeshi la Polisi.
Makao
Makuu ya Polisi.
No comments:
Post a Comment