Jesca Msambatavangu. |
IRINGA.
KAMATI za Maadili Chama cha Mapinduzi (CCM) ngazi mbalimbali
mkoani Iringa zinaanza kukutana leo Jumatatu Desemba 28, kusikiliza ushahidi
toka kwa wanaCCM wanaodaiwa kukisaliti chama hicho wakati wa uchaguzi Mkuu ambao
ulifanyika Oktoba 25 mwaka huu.
Mmoja wa watakaoitwa na kamati hizo ni Mwenyekiti wa CCM wa
mkoa huo, Jesca Msambatavangu na Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa,
Mahamudu Madenge.
Msambatavangu na Madenge wanatuhumiwa pamoja na wasaliti
wengine 30 wa mjini Iringa, kukisaliti na kukihujumu chama hicho hadi
kikapoteza ubunge kwa mara nyingine tena kwa Mchungaji Peter Msigwa wa Chama
Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na kikanyang’anywa kata 14, walizokuwa
wakizishikilia CCM kwa miaka yote.
Kwa upande wake, Msambatavangu ambaye mara kwa mara
amenukuliwa akipinga kuhusika katika tuhuma hizo, amesema yupo tayari kutoa
ushirikiano kwa kamati hizo na akawataka watuhumiwa wengine wafanye hivyo, ili
kumaliza suala hilo linalozidi kukigawa chama hicho mkoani humo.
No comments:
Post a Comment