Friday, June 14, 2013

BAJETI CHUNGU: SIMU ZA MKONONI KUPIGWA USHURU




Simu ya mkononi.


















Dodoma, 
Tanzania.

WAMILIKI wa simu za mkononi nchini kuanzia mwezi ujao wataanza kuingia gharama kubwa ya kumiliki simu zao, baada ya serikali kuweka ushuru wa asilimia 14.5 ili kuongeza mapato ya Serikali na kugharamia elimu.

Kutokana uamuzi wa serikali sasa mmiliki wa simu atalazimika kutumia fedha nyingi kuigharamia ikiwa ni pamoja na kulipa fedha za kuchangia elimu achilia mbali kulipia muda wa hewani, na gharama nyingine ambazo mtu au watu wamekuwa wakikatwa na kampuni za simu kwa mfano nyimbo na ghama nyingine.

Waziri wa Fedha na Uchumi, Dkt. William Mgimwa amesema hayo wakati akiwasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2013/14 unaonaza Julai Mosi mwaka huu.


Dkt. Mgimwa amesema kila mmiliki wa simu atalazimika kulipa kiasi hicho kwa kila kadi ya simu kwa mwezi na ushuru huo utakusanywa na kampuni za simu nchini.

Katika eneo hilo pia, Waziri Mgimwa alisema Serikali inakusudia kuanzia mwezi ujao kutoza ushuru wa bidhaa wa asilimia 14.5 kwenye huduma zote za simu za kiganjani, badala ya muda wa maongezi peke yake.

“Katika ushuru huu asilimia 2.5 zitatumika kugharamia elimu hapa nchini.............hatua hii imezingatia mapendekezo ya Kamati Maalumu ya Spika ya Kushauri kuhusu mapato na matumizi ya Serikali,” alisema Dkt. Mgimwa.

No comments: