Monday, June 24, 2013

MANDELA MAHUTUTI HOSPITALINI
















Afrika Kusini. 

MADAKTARI wanaomtibu rais wa zamani wa Afrika Kusini, Mzee Nelson Mandela wamesema hali yake imekuwa sio nzuri kwa saa 24 zilizopita na sasa ni mahututi.

Habari hizo zimekuja kupitia taarifa iliyotolewa na ofisi ya rais ya Afrika Kusini.

Taarifa hiyo imesema bado Mzee Mandela ameendelea kusalia hospitalini mjini Pretoria kwa siku ya kumi na sita akitibiwa mapafu yaliyosababisha tatizo kwenye mfumo wake wa upumuaji.

Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma amemtembelea Mzee Mandela jumapili jioni na kuzungumza na jopo la matatibu wanaomtibia.

Baadaye bwana Zuma alirejea kauli yake ya kulitaka taifa na dunia kumuombea Mzee Mandela apate nafuu.(BBC Swahili News).

No comments: