Friday, June 28, 2013

SHILINGI BILIONI 161 KUTUMIKA ULINZI WA SAFARI YA OBAMA AFRIKA

Rais Obama.
















Marekani. 

SAFARI ya siku nane ya Rais wa Marekani, Barack Obama katika nchi tatu za Afrika Senegal, Afrika Kusini na Tanzania  itaigharimu kati ya dola 60 na 100 ambazo ni sawa na kati ya Shilingi 161 bilioni na Shilingi 161 bilioni kwa ajili ya kuhakikisha Rais Barack Obama anapewa ulinzi wa hali ya juu.

Kiasi hicho cha fedha ni gharama za malazi,chakula pamoja na mambo mengine. Kwa mujibu wa wataalamu wa masuala ya uchumi wamesema fedha hizo zingilitosha kwa matumizi ya wizara tatu za Tanzania katika mwaka mmoja lakini kwa kuzingatia bajeti ya mwaka 2013/14 ambayo imetishwa juzi bungeni.

Kwa mujibu wa bajeti hiyo, Wizara au Ofisi ya Makamu wa Rais Shilingi 55.6 bilioni, Wizara ya Maliasili na Utalii Shilingi 75.6 bilioni na Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Shilingi 30.3 bilioni.


Ziara ya Obama imeanza rasmi katika Jiji la Dakar nchini Senegal, baadaye Jonannsburg na Cape Town nchini Afrika Kusini na mwisho ziara yake itakuwa ni Tanzania, Julai Mosi, mwaka huu.

Gazeti la Washington Post la Marekani, limebainisha kwamba fedha hizo zitatumiwa na idara ya usalama za Marekani ili kuhakikisha usalama wa Rais Obama.

Washington Post limesema mashushu wengi wametumwa Tanzania, Senegal na Afrika Kusini kwa ajili ya kuhakikisha Obama anakuwa katika mikono salama.

Pia gazeti hilo limeeleza kwamba manowari ya kijeshi itawekwa katika Pwani ya Afrika Mashariki kwa ajili ya kukabiliana na dharura yoyote. Manowari hiyo ina kituo cha kutoa matibabu.

Kwa mujibu wa gazeti hilo, ndege za kijeshi za mizigo zitabeba magari 56 ya msaada, magari 14 aina ya Limousines na malori matatu yenye vioo maalum vya kuzuia risasi ambavyo vitawekwa kwenye hoteli ambako ataishi rais Obama.

No comments: