Thursday, June 13, 2013

MAJI CHANZO CHA WANAWAKE KUBAKWA

 



















Mwanamke akichota maji machafu kwa ajili ya matumizi ya nyumbani, kutokana na uhaba wa maji. (Picha kwa hisani ya Fullshangweblog)
















Na Mwandishi wetu,

WANAWAKE pamoja na watoto wa kike wa mkoa wa Shinyanga  Jimbo la Kishapu kata ya Mnhunze nchini Tanzania wanakabiliwa na matatizo ya kubakwa na kupigwa, kwa sababu ya shida ya maji.
Mbali na matukio hayo pia wamekuwa wahanga wa kupigwa na waume zao baada ya kuchelewa kurudi jumbani kutokana na kwenda umbali mrefu kutafuta maji.

Wakizungumza na mwandishi wetu, wanawake wa vijiji vya Mnhunze, Kisoso na Lubago wamesema kwamba mateso hayo pia wanakabiliwa na mlipuko wa magonjwa ya kuambukiza kwa sababu ya kutumia maji yasiyostahili kwa matumizi ya binadamu ili kuepuakana na shida matatizo hayo hayo.


"Tunalazimika kuamka saa tisa za usiku kutafuta maji baada ya tatizo hili kuzungumziwa  mara kwa mara bila mafanikio yoyote yanayoonekana"alisema   Anastazia Christopher mkazi wa kijiji cha Isoso.

Paskazia John mkazi wa kijiji cha Lubaga katika kata  ya Mnhunze alielezea machungu anayoyapata juu ya janga hilo kubwa la maji linalowakabili wakazi wa kijiji chao na kudai kwamba linamnyima raha kutokana na baada ya kuwa chanzo  cha kuleta matatizo ya kifamilia katika jamii yao.

"Mambo mengi sana yanatokea kutokana na tatizo hili la ukosefu wa maji kwani maji yanapatikana mbali sana na inawalazimu kuamka saa tisa usiku ili waweze kuyapata maji,pia imesababisha madhara makubwa sana kwa watoto wao wa kike", alisema John.

No comments: