Friday, June 28, 2013

WAANZA MAANDALIZI YA UJENZI WA KABURI LA MANDELLA

Mzee Nelson Mandella Madiba.

Pretoria,
Afrika Kusini. 

SERIKALI ya Afrika Kusini imeanza kuandaa mahali ambako rais wa zamani wa nchi hiyo atazikwa,  sambamba na ndugu kuelezwa kwamba wana haki ya kuondoa au kusimamisha mashine inayomsadia mzee huyo kuendelea kuishi.

Tayari gari linalotumika kuchimba makaburi limepelekwa kwenye eneo la makaburi ambako Mandela anatarajiwa kuzikwa. 

Lakini mbali ya hilo familia na maofisa wa serikali wamewasili nyumbani kwa Mzee Mandela, Qunu.

Kutokana na hali ya Mzee Mandela,  nchini Afrika Kusini hivi sasa kumekuwapo kwa shughuli nyingi nyumbani kwake, eneo la Qunu na pia katika Hospitali ya Pretoria ambako Madiba amelazwa kwa matibabu na makazi yake ya zamani-Mtaa wa Vilakazi, Soweto, pia mtaa kuko bize.


Jumanne wiki hii, machifu na maofisa wa serikali walikwenda katika familia ya Mandela na kukutana na ndugu hao kwa karibu masaa mawili na baada ya kutua kwenye Uwanja wa Ndege. Baadaye machifu hao walielekea katika eneo la Mathatha.

Mmoja wa maofisa wa serikali alikuwa ni Waziri wa Utumishi na Utawali, Lindiwe Sisulu na kiongozi wa UDM, Bantu Holomisa ambao wameshiriki katika mazungumzo hayo kwa ajili ya maandalizi ya mazishi.

Maofisa hao walikutana na mjukuu wa Mzee Mandela, Ndaba Mandela na baadaye walikwenda kukagua mahali pa kuchimba kaburi. Baadaye wachimbaji wa kaburi waliwasili kwenye eneo hilo baada ya masaa mawili. Kwa mujibu wa mtandao wa News 24, gari hilo limepaki meta 150 kutoka eneo la makaburi hayo.

Wakati hayo yakitokea, ndugu wa Mzee Mandela au Madiba wameambiwa kwamba wana haki ya kuamua kuiondoa mashine inayomsadia kuishi.

Mzee Mandela anaishi kwa kutumia mashine na imeelezwa kwamba figo zake zinafanya kazi chini ya asilimia 50.

Katika eneo la Jimbo la Mashariki ya Afrika Kusini, ambako Madiba alikulia huko, kiongozi wa kimila amesema muda wa Mzee Mandela umefika.

“Kwa maoni yangu kama Madibayu mahututi na sasa anaishi kwa kutumia mashine na hakuna anayethamini, Mungu afanye uamuzi ili kumuondolea mateso anayupata sasa,” amesema chifu Phathekile Holomisa.

No comments: