Saturday, October 5, 2013

SAKATA LA WEZI KUVAMIA IKULU NDOGO WILAYANI MBINGA: ASKARI WAWILI WAHOJIWA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete.




















Na Kassian Nyandindi,
Ruvuma.

JESHI la polisi mkoani Ruvuma, linawahoji askari wake wawili ambao wanadaiwa kuzembea wakiwa lindoni, na kusababisha watu wasiojulikana ambao ni wezi kuvamia eneo la Ikulu ndogo wilayani Mbinga mkoani  humo, na kufanya uhalifu.

Ikulu ndogo wilayani humo ndiyo ambayo anaishi Mkuu wa wilaya hiyo Senyi Ngaga, huku baadhi ya wakazi wa mji wa Mbinga kufuatia tukio hilo wamesema kwa nyakati tofauti kwamba, kuna kila sababu katika eneo hilo kutofanyiwa mzaha na kuwepo na ulinzi wa kutosha kwa askari ambao waaminifu.

Uhalifu uliofanywa na wezi hao ni kwamba walitoboa ukuta wa chumba ambacho kuku hao walihifadhiwa, ambapo inadaiwa kuwa askari waliokuwa lindoni hawakuwa makini katika kutimiza majukumu yao.

Wezi hao baada ya kuvamia katika eneo hilo Oktoba 2 mwaka huu majira ya usiku, walifanikiwa kutoboa ukuta huo wa kibanda ambacho kimejengwa kwa tofari, na kuiba kuku saba kati ya 28 ambao walikuwemo ndani yake.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Ruvuma, Deusdedith Nsimeki amethibitisha kuhojiwa kwa askari hao ambao majina yao hakuyataja, na kuongeza kuwa taarifa kamili juu ya tukio hilo, itatolewa baadaye mara baada ya uchunguzi kukamilika.

No comments: