Na Kassian Nyandindi,
Mbinga.
MTUHUMIWA ambaye alikuwa akishikiliwa katika Kituo kikuu cha
Polisi wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma, Bosco Ndunguru (40) amekutwa akiwa
amefariki dunia baada ya kujinyonga kwa kutumia shati ambalo alikuwa amelivaa,
wakati alipokuwa kwenye mahabusu ya kituo hicho cha polisi wilayani humo.
Ndunguru aliwekwa mahabusu, kwa tuhuma ya kuvunja jengo la
polisi na kuiba Radio call ya kituo hicho mwaka jana, ambapo alitoroka
kusikojulikana na Jeshi hilo lilikuwa likimtafuta kwa muda mrefu.
Taarifa zinaeleza kuwa tukio hilo lilitokea Januari 23 mwaka
huu majira ya asubuhi, ambapo baada ya kukamatwa na kuswekwa rumande ilikuwa afikishwe
Mahakamani kwa ajili ya kujibu tuhuma, ambazo zilikuwa zinamkabili.
Imedaiwa kuwa mtuhumiwa huyo baada ya kuingizwa mahabusu,
muda mwingi alikuwa akilia na kulalamika sana, huku akidai kuwa ndugu zake
hawampendi.