Thursday, April 16, 2015

AWEZAE AFARIKI DUNIA KWA KUGONGWA NA LORI TUNDURU

Na Mwandishi wetu,
Tunduru.

AWEZAE Mohamed (35) amefariki dunia kufuatia ajali mbaya iliyotokana na pikipiki ambayo alikuwa akisafiria, kugongwa na lori aina ya Steya lenye namba za usajili T 862BFW ambalo linatumiwa kubeba kifusi cha udongo.

Kadhalika mume wake Issa Swalehe naye amelazwa katika Hospitali ya wilaya ya Tunduru kufuatia ajali hiyo, ambaye ni mlinzi katika kampuni ya kichina ambayo inajenga barabara kutoka Tunduru mjini hadi kata ya Matemanga wilayani humo.

Tukio hilo lilitokea Aprili 3 mwaka huu, kijiji cha Amani katika kata ya Nandembo wilayani humo ambapo marehemu huyo alikuwa akisafiria pikipiki aina ya Sunlg yenye namba za usajili T 886 CTC ambayo ilikuwa ikiendeshwa na mumewe huyo.


Kaimu kamanda wa polisi wa mkoa wa Ruvuma, Revocatus Malimi alisema chanzo cha ajali hiyo, bado hakijafahamika na kwamba dereva wa lori hilo Rashid Shaban ametokomea kusikojulikana na polisi bado wanamtafuta.


Akizungumza kwa shida, majeruhi Ngulinga ambaye amelazwa wodi namba tatu katika hospitali ya wilaya hiyo alisema, chanzo cha ajali hiyo ni uzembe uliofanywa na dereva wa lori hilo, baada ya kuwaruhusu wapite ndipo waligongana.

No comments: