Na Mwandishi wetu,
Iringa.
SERIKALI imepata mkopo wa Sh. bilioni 15 kulipa madeni ya
mazao ya nafaka ambayo wakulima wanaidai kupitia Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya
Chakula (NFRA).
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, alisema hayo wakati
akizungumza na wananchi wa Mkoa wa Iringa akiwa kwenye ziara ya kikazi ya
kukagua maendeleo mkoani humo.
Akizungumza baada ya kukagua Chama cha Ushirika cha Akiba na
Mikopo (SACCOS) cha Mazombe, kilichopo Ilula, wilaya ya Kilolo, mwishoni mwa
wiki iliyopita, Pinda alisema katika kipindi cha mwezi huu, serikali imepata
mkopo huo kutoka Benki ya CRDB na kusambazwa kwenye mikoa mbalimbali ili
kuwalipa wakulima hao.
Alisema hadi kufikia Machi, mwaka huu, serikali itahakikisha
inamaliza kulipa madeni kwa wakulima waliouza mazao yao kwa NFRA.
No comments:
Post a Comment