Kikosi maalum cha Halaiki-Makomandoo wenye umri mdogo,
kikiwa kimebeba silaha za SMG kinapita mbele ya Mwenyekiti wa CCM, kumuonesha
umahiri wao.
Dokta Emmanuel
Nchimbi atoa hotuba:
Ndugu Mwenyekiti, uliagiza ujenzi wa barabara ya Manispaa bado haujatekelezwa,
pia uliagiza wakulima wadogo wadogo wapewe kipaumbele kisha mawakala na ulitoa
pesa takribani bilioni 7.7, tunakushukuru sana.
Mhe Rais, Wananchi wa Songea wanapenda sana mpira na wana timu yao ya majimaji,
nimepata mdau kutoka marekani aliyetuchangia Milioni 150, hivyo kwako rais
hatutaki chochote zaidi ya dua tu. (makofi).
Oddo Mwisho Azungumza:
Mwenyekiti wa CCM
mkoa wa Ruvuma, Oddo Mwisho alianza kwa kusema; tunakushukuru Mheshimiwa
JK, kwa kutuletea sherehe hizi Ruvuma wananchi wa Ruvuma wanawakaribisha sana.
CCM inajivunia
wingi wa wanachama laki 257 456. Hakuna mbunge wa upinzani katika mkoa huu.
Tunakuhakikishia sisi wananchi kwa umoja wetu CCM itashinda kwenye uchaguzi
mkuu 2015. Kwa ushahidi, tumeshinda kwa asilimia zaidi ya 90 kwenye uchaguzi wa
serikali za mitaa.
Kapteni Komba:
Kapteni Komba
aliitwa kutumbuiza kidogo ili kumkaribisha Mwenyekiti wa CCM, Jakaya Kikwete
kuzungumza, kisha baada ya hapo, alifuatia mwanamuziki wa bongo fleva, Diamond
Platnum kutoa burudani.
Kinana:
CCM oyeee! nani
kama CCM? nani kama Kikwete?
Ndugu Mwenyekiti kabla sijakukaribisha, nachukua nafasi hii kuwashukuru
wanaruvuma kwa maandalizi na kuwakaribisha wageni kutoka chama cha National
Resistance Movement (NRM) kutoka Uganda.
Katibu mkuu NRM,
Jestine Lumumba alitoa neno la shukrani. (Anashangiliwa).
Sasa Kinana anawatambulisha zaidi wajumbe kutoka Uganda, Rose Nyamayanja, John
kiangi na wengineo.
Katibu huyo wa
CCM, sasa anamkaribisha makamu Mwenyekiti wa chama cha NRM kusema machache.
Makamu Mwenyekiti wa NRM:
CCM oyee, CCM
itaendelea kutawala (makofi na vifijo kwa wingi).. Tunafurahi sana kuwepo ndani
ya nchi ya Tanzania. Vijana mpo? CCM juu..
Ndugu zangu sisi tumetoka Uganda kuungana na CCM kama NRM tuko pamoja Ndugu
Mwenyekiti mnamo miaka ya 1970 Nyerere alisema kwamba “Watanzania, adui
imetuingilia, na sisi watanzania, hatuna chochote cha kufanya, kilichobaki ni
kumpiga nyoka. Sababu tunayo, uwezo tunao na nia ya kumpiga nyoka tunayo''.
Nataka kusema kwamba, siku hiyo ndiyo sisi tuliamua kuungana na Tanzania.
Tunakumbuka ukombozi wa Uganda. Leo tumesimama imara kama nchi na Tanzania imetusaidia
sana.
Rais Museven na familia yake ilikuwa Tanzania, mfumo wa uongozi tumekopi
Tanzania, ukombozi wa South Afrika, Zimbabwe, Angola, Namibia ulianzia
Tanzania.
Tunakumbuka sana, mzigo Tanzania ilioubeba ilitokea ndani ya chama cha CCM.
Mwisho nasema, muungano wa Afrika Mashariki ulianzia hapa Tanzania. Niseme
kwamba, Muungano wa Afrika Mashariki udumu! Tutahakikisha nchi zote za Afrika
Mashiriki tutakuwa nchi moja. Nasema asante sana Tanzania, Hongera CCM kuongoza
miaka 38.
Mungu Ibariki Tanzania. Tuko pamoja. Rais Kikwete Juu, Rais Museven juu.....
|
No comments:
Post a Comment