Na Mwandishi wetu,
Songea.
WAFANYABIASHARA waliopo katika Manispaa ya Songea, mkoani
Ruvuma wamewataka wabunge wa mkoa huo, warudi kwenye majimbo yao ili
waweze kujadili changamoto inayowakabili wafanyabiashara hao, juu ya ongezeko
la kodi mara mbili na kiwango kilichokuwa kikitozwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania. (TRA)
Akizungumza katika mkutano
uliyofanyika kwenye ukumbi wa Songea Club uliopo mjini hapa, Mwenyekiti wa
wafanyabiashara hao, Isaya Mbilinyi alisema kuwa ongezeko hilo limefikia
asilimia 100 jambo ambalo, linalowafanya wafanyabishara wengi kushindwa kumudu
gharama ya ulipaji wa kodi.
Mbilinyi alisema kuwa kutokana na Bunge kupitisha kiwango
hicho cha ulipaji kodi, ni vyema wabunge wa majimbo ya mkoa wa Ruvuma
warudi na kukaa pamoja na wafanyabiashara hao ili waweze kujadili
na kutambua changamoto hiyo ambayo inawakabili.
“Tuanawaomba wabunge
wetu tukae pamoja kujadili suala hili, kabla bunge halijapitisha kuwa sheria
ambalo kwa sasa bado limekuwa kwenye mswada kwa kuwa wafanyabiashara
tulio wengi, vipato vyetu ni vya chini ambavyo haviwezi kumudu ongezeko hilo la
kodi hiyo,
“Wafanyabiashara wenzangu suala hili lisiwe la ugomvi,
kinachotakiwa tuendelee kupaza sauti kwa kufuata taratibu zinazotakiwa ili
mwisho wa siku serikali iweze kutusikiliza, ndio maana tunaanza na wabunge wetu
ambao ni wawakilishi wetu,” alisema Mbilinyi.
Kwa upande wake Meneja wa TRA mkoa wa Ruvuma, Apili Mbaruku
alisema ofisi yake haina uwezo wa kutengua mambo yaliyoopitishwa na bunge, bali
bunge hilo ndilo lenye nafasi ya kuweza kujadili na kuamua maamuzi mengine.
No comments:
Post a Comment