Na Steven Chindiye,
Songea.
KATIKA uchaguzi mkuu ujao ambao unatarajiwa kufanyika hapa
nchini, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeendelea kutamba kuibuka na ushindi
mnono katika chaguzi hizo, ambazo zitahusisha Madiwani, Wabunge na Rais mwezi
Oktoba mwaka huu.
Nape Nnauye ambaye ni Katibu wa Itikadi na Uenezi taifa wa
chama hicho, alitoa kauli hiyo alipokuwa akizungumza kwenye maadhimisho ya kitaifa
miaka 38 ya kuzaliwa kwa chama cha mapinduzi, yaliyofanyika uwanja wa Majimaji
Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma.
NNauye ambaye alionesha kurusha vijembe hivyo kwa vyama vya upinzani
akisema, kilichofanywa na CCM katika chaguzi za serikali za mitaa ilikuwa ni
mvua za rasha rasha na kwamba katika uchaguzi mkuu Oktoba mwaka huu, wapinzani
hawata ambua kitu.
“Tayari ng’ombe amekwisha lala kibra hivyo lazima
achinjwe”, alisema Katibu huyo.
Awali wakitoa burudani kwa wananchi waliofurika mjini Songea
kwenye uwanja wa Majimaji, wakiwemo wapenzi na wakereketwa wa chama cha
mapinduzi, bendi ya TOT inayomilikiwa na chama hicho, walikuwa wakiimba wimbo
wa kupongezwa kwa utekelezaji wa sera za chama huku watu wengi wakishangilia na
kufurahi.
Katika wimbo huo pamoja na mambo mengine, walitaja
baadhi ya mafanikio yaliyotekelezwa na chama tawala kupitia serikali yake ya awamu
ya nne kuwa kimejenga shule nyingi, hospitali, vituo vya afya na zahanati ikiwa
ni juhudi ya kuhakikisha wananchi wake wanapatia huduma nzuri.
Mwenyekiti CCM Taifa
naye azungumza:
Mwenyekiti wa Chama hicho Dokta Jakaya Kikwete, wakati akihutubia
maelfu ya wanachama na wakereketwa wa CCM waliojitokeza kushiriki maadhimisho
hayo, alisema, “dalili ya mvua ni mawingu kwani ushindi mkubwa kilioupata chama
cha mapinduzi CCM katika uchaguzi wa serikali za mitaa, ni kielelezo
tosha cha ushindi mwaka huu”.
Dokta Kiwete, amewataka wanaccm wasibweteke kwa ushindi
huo, badala yake waunganishe nguvu zao kwa kufanya kazi pamoja, ili
kujihakikishia ushindi huo unapatikana tena katika uchaguzi ujao.
Alifafanua kuwa huu ni mwaka ambao lazima kazi ya jumuiya za
chama cha mapinduzi, zinazokiwezesha chama hicho kushinda, lazima zifanye kazi
zinazo onekana na kuonesha dira katika ushindi wa chaguzi zijazo.
Kadhalika aliwataka viongozi wa CCM waliopo madarakani,
kujipima kuwa wapo katika kundi gani katika utekelezaji wa yale waliyoahidi kwa
wananchi huku akiongeza kuwa mwaka huu, ni mwaka wa uchaguzi ambao wapiga kura
watawahukumu viongozi waliopo madarakani kwa mambo waliyoyatekeleza ambayo
walitoa ahadi kwa wananchi wao, katika uchaguzi mkuu uliopita.
No comments:
Post a Comment