Na Steven Augustino,
Tunduru.
MKUU wa wilaya ya ya Tunduru mkoani hapa, Chande Nalicho
ametoa wiki mbili kwa wazazi wilayani humo, wahakikishe kwamba wanawapeleka
watoto wao ambao wamechaguliwa kujiunga na masomo ya sekondari kidato cha kwanza
mwaka huu, na kwa asiye tekeleza hilo hatua kali za kisheria zitachukuliwa
dhidi yake.
Nalicho alitoa kauli hiyo, wakati alipokuwa akitoa salamu za
serikali kwenye kikao cha baraza la Madiwani wa halmashauri ya wilaya hiyo,
kilichofanyika ukumbi wa Klasta ya walimu mlingoti mjini hapa.
Akifafanua taarifa yake, Mkuu huyo wa wilaya alisema maagizo
hayo ameyatoa kufuatia kuwepo kwa idadi kubwa ya wanafunzi ambao hawajaripoti
katika shule walizochaguliwa kwenda kusoma, huku takwimu zikionesha ni asilimia
tano tu ndio waliokwenda kuripoti na kuanza masomo kati ya asilimia 54.1 ya
watoto wote waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza.
Kutoripoti kwa watoto hao, kunaondoa sifa kwa wilaya hiyo
kufanya vizuri katika matokeo ya mtihani wa darasa la saba.
Alisema katika matokeo hayo wilaya yake imefaulisha watoto 2,573
ambapo kati yake, wavulan ni 1,403 na wasichana 1,173 ikiwa ni tofauti na mwaka
2014 ni zaidi ya mara mbili, ambapo wilaya ilifaulisha watoto 1,364 na kushika
nafasi ya mwisho kiwilaya.
Sambamba na agizo hilo la Nalicho, kadhalika aliwataka
madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Tunduru kuongeza nguvu katika kuendelea na
uhamasishaji wa ujenzi wa maabara, katika shule za sekondari wilayani humo na
kuhakikisha ujenzi wake unakamilika kwa wakati.
No comments:
Post a Comment