Rais Jakaya Kikwete. |
Na Mwandishi wetu,
Tunduru.
WAKUU wa wilaya wateule, ambao wanakwenda kuchukua nafasi ya
mkuu wa wilaya ya Mbozi, Ahamad Namohe na Mariam Jumaa aliyepangiwa kwenda
wilaya ya Lushoto, kwa nyakati tofauti wamewataka wananchi wa wilaya hizo
kutoa ushirikiano wa kutosha kwao, ili waweze kusimamia kikamilifu shughuli za
kimaendeleo wakati watakapokuwa katika maeneo hayo.
Sambamba na maelezo hayo, pia wateule hao walisema
watazingatia wanatekeleza majukumu yao ya kazi kwa kuhakikisha hawata muangusha, Rais Jakaya
kikwete ambaye aliwateua katika kutekeleza na kusimamia maendeleo ya wananchi
wake hususani kwenye nyanja ya elimu, afya na maji na mambo mengine mengi huko
waendako.
Aidha katika mahojiano hayo, walitumia nafasi hiyo kumpongeza
Rais huyo kwa kuwaona na kuwaamini kuwa wanao uwezo, wa kuitumikia nchi yao.
“Nafasi niliyopewa ni adimu sana, binafsi nina amini kuwa
kazi niliyopangiwa nitaifanya kwa uangalifu na uaminifu mkubwa, na kuhakikisha wilaya
ninayokwenda inapiga hatua mbele kimaendeleo,” alisema Namohe.
Pamoja na mambo mengine, wakuu hao wa wilaya walionesha kujiamini
katika maelezo yao wakisema kuwa kazi wanazoenda kufanya, hazina tofauti na
kazi za uafisa tarafa walizokuwa wakizifanya, katika maeneo yao wilayani
Tunduru.
“Hakuna kazi ngeni kwetu, kwani wakati tukiwa maafisa tarafa
tulikuwa tunafanya vikao vya kujadili hali ya ulinzi katika kata zetu na
kuhakikisha amani na maendeleo yanapatikana sehemu husika”, alisisitiza Mariam.
No comments:
Post a Comment