Na Amon Mtega,
Songea.
WATU wanaotumia dawa za kurefusha maisha (ARV) mkoani Ruvuma,
wametakiwa kufuata maelekezo ya watalaamu wao, namna ya kutumia dawa hizo na
kuachana na maelekezo yanayotolewa na watu wengine mitaani, ili waweze kuepukana
na madhara yanayoweza kutokea baadaye.
Wito huo ulitolewa na Mratibu wa magonjwa ya kifua kikuu na UKIMWI,
wilaya ya Songea mkoani humo, Adam Ngunga kwenye mafunzo elekezi kwa wanachama zaidi
ya 80 kutoka sehemu mbalimbali mkoani Ruvuma, wa shirika lisilokuwa la kiserikali
(DMI) yaliyofanyika mjini hapa.
Wanachama hao walielekezwa namna ya kuepukana na maambukizi
ya ugonjwa huo, pamoja na matumizi ya dawa za ARV kwa mgonjwa ambaye tayari
anastahili kutumia dawa hizo, mara baada ya kushuka kwa kinga zake
mwilini.
Mafunzo hayo yalieandana na wanachama kupima afya zao na
kuwataka huko waendako wakaelimishe jamii, juu ya matumizi sahihi ya dawa za
UKIMWI ili kuondokana na malalamiko yasiyokuwa na msingi ambayo hujitokeza
miongoni mwa jamii, hasa pale mgonjwa anapozembea kutumia dawa hizo.
Ngunga alisema, hali hiyo imekuwa ikiwasumbua wengi wao ambao
hupuuza maelekezo ya watalaamu, na kuwafanya kuwepo kwa mabadiliko ndani ya
miili yao na kuchukia dawa ambazo huzitumia, huku wengine wakipoteza maisha.
Alifafanua kuwa pamoja na kuwepo kwa baadhi ya watu kupuuzia
maagizo yanayotolewa na daktari, pia amewataka wajenge utamaduni wa kupima afya
zao mara kwa mara, ili waweze kujitambua na kufanya maamuzi yaliyo sahihi katika
maisha yao ya kila siku.
No comments:
Post a Comment