Mkuu wa wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma, Chande Nalicho akipokea miche ya mikorosho bora kutoka kwa Mwenyekiti wa mfuko wa kuendeleza zao la korosho Tanzania, Athuman Nkinde.
(kushoto)
|
Mkuu wa wilaya ya Tunduru Chande Nalicho, akimkabidhi miche ya mikorosho kaimu mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya hiyo, Chiza Marando wa upande wa kulia kwa ajili ya
kuisambaza kwa wakulima.
|
Namtumbo.
Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma, imepongeza
juhudi za Mfuko wa Kuendeleza zao la Korosho Tanzania (WAKFU) kwa
kuwapatia mgao wa mikorosho mipya, ikiwa ni juhudi ya serikali kuinua kipato
kwa wananchi wake na kuendeleza kilimo cha zao hilo.
Hayo yalisemwa na wawakilishi wa halmashauri hiyo, akiwemo
kaimu afisa kilimo wa wilaya hiyo, Aniseth Ndunguru na mratibu wa zao hilo Joseph
Ngatunga wakati wakikabidhiwa miche mipya 10,000 ya korosho.
Aidha viongozi hao kwa niaba ya halmashauri hiyo, pamoja na
pongezi hizo pia walimhakikishia Mwenyekiti wa mfuko wa kuendeleza zao hilo
Tanzania, Athuman Nkinde kwamba, wapoimara katika kuwawezesha wakulima kielimu juu
ya kilimo cha zao hilo, pamoja na kuisambaza kwa wingi kwa wakulima wao.
Walisema katika kipindi cha msimu wa kilimo mwaka 2014,
halmashauri ilipokea miche bora 10,000 yenye thamani ya shilingi milioni 55 ambayo
iliyotolewa na mfuko huo.
Akifafanua mbele ya Mwenyekiti wa mfuko huo, Ngatunga alisema
kuwa kiasi cha mikorosho ambayo wamegawiwa wakulima kwa msimu huu, pia
imepangwa kusambazwa tena kwa wakulima waliopo kata za Ligela, Mchomoro, Limamu
na Likuyuseka.
Awali akimkabidhi miche ya mikorosho hiyo, Mwenyekiti huyo wa
WAKFU Athuman Nkinde alieleza mfuko huo, umedhamiria kutekeleza kwa vitendo
kauli mbiu ya kilimo kwanza.
Alisema mikorosho hiyo inatakiwa kusambazwa na kugawiwa bure
kwa wakulima wote nchini, kutokana na tayari mfuko kugharimia gharama zote za
uendeshaji juu ya zoezi hilo.
Miche hiyo husambazwa kwa wakulima baada ya kufanyiwa usanifu
na Wataalamu wa mimea, kutoka kituo cha utafiti cha Naliendele ambacho kimeweka
matawi yake katika wilaya ya Tunduru, kinacho hudumia kanda ya kusini, Mpwapwa
kinachohudumia wakulima kanda ya ziwa na Mkuranga kinahudumia wakulima wa kanda ya Mashariki na Kaskazini.
Aliendelea kueleza kuwa sambamba na ongezeko la uzalishaji
huo, pia mfuko umeandaa utaratibu wa kugawa mashine maalumu kwa ajili ya kuwasaidia
No comments:
Post a Comment