Saturday, February 28, 2015

BREAKING NEWS: KAPTENI JOHN KOMBA MBUNGE WA MBINGA MAGHARIBI AFARIKI DUNIA

Kapteni Komba, akiwajibika jukwaani kwenye bendi ya TOT enzi ya uhai wake.


Na Mwandishi wetu,
Dar.

TAARIFA za uhakika zilizotufikia hivi punde, kutoka kwenye chumba chetu cha habari zinaeleza kuwa, aliyekuwa Mkurugenzi wa Tanzania One Theater (TOT) na Mbunge wa jimbo la Mbinga Magharibi mkoani Ruvuma, Kapteni John Komba (pichani) amefariki dunia.

Kapteni Komba amefariki dunia jioni hii, katika Hospitali ya TMJ Mikocheni Jijini Dar es Salaam, ambako alikuwa amelazwa akipatiwa matibabu.

Mtoto wake, Jerry Komba amesema chanzo cha kifo cha baba yake ni kushuka kwa sukari akiwa nyumbani kwake Mbezi, ambapo baada ya kukumbwa na tatizo hilo walimpeleka katika hospitali hiyo, kwa ajili ya matibabu zaidi na ambako mauti yalimkuta.

Thursday, February 26, 2015

TASAF YAPINGA VITENDO VYA UPOTOSHWAJI JUU YA SHUGHULI ZAKE


Na Steven Augustino,

Njombe.

TAARIFA potofu kuhusu yale yanayofanywa katika awamu ya tatu, katika mpango wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii Tanzania (TASAF) kwamba umezifanya baadhi ya kaya maskini hapa nchini, zinazokidhi vigezo vya kuwezeshwa kiuchumi kuwa zimekosa fursa ya kunufaika na mpango huo, imeelezwa kuwa sio kweli bali ni upotoshaji katika jamii.

Mkurugenzi mtendaji wa TASAF, Ladislaus Mwamanga alisema mpango huo ulizinduliwa Agosti 15 mwaka 2012 na Rais Jakaya Kikwete na kuanza kutekelezwa Februari 2013 ambapo unalenga kuzinusuru kaya masikini, kwa kuzisaidia fedha ili zipate huduma mbalimbali ikiwemo elimu, afya na maji.

Akifungua kikao cha kazi cha siku mbili mjini Njombe jana, ambacho kimewashirikisha waratibu wa mpango huo, wahasibu, maafisa ufuatiliaji na wanahabari, Mwamanga alisema baadhi ya kaya maskini zimekuwa zikidanganywa kwamba fedha zinazotolewa kupitia mpango huo ni za Freemasons.

VIONGOZI WATAKIWA KUJIPIMA NINI WAMELIFANYA KATIKA TAIFA HILI


Na Nathan Mtega,

Songea.

IMEELEZWA kuwa viongozi wa ngazi mbalimbali nchini, wametakiwa kujipima katika utendaji wao wa kuwatumikia wananchi pamoja na wanaowaongoza kama wanatekeleza majukumu yao ipasavyo, kwa uadilifu na moyo wa uzalendo katika taifa hili kama walivyofanya wa asisi wetu akiwemo, Hayati Rashid Mfaume Kawawa.

Katibu tawala wa mkoa wa Ruvuma, Hassan Bendeyeko alisema hayo wakati alipokuwa akifungua tamasha la kumuenzi Hayati Rashid Kawawa linaloenda sambamba na kuwakumbuka mashujaa wa vita ya Maji maji, yanayofanyika mjini Songea mkoa humo ambayo yameanza kwa wajumbe wa kamati hiyo ya maandalizi inayofanya kazi chini ya Mwenyekiti wake, Fredrick Mwakalebela kwa kutembelea baadhi ya maeneo ambayo muasisi huyo aliishi na kufanya kazi mkoani hapa.

Alisema ni vyema wakati taifa linawakumbuka viongozi na waasisi wake pamoja na mashujaa wa vita hiyo, ambayo ndiyo ilikuwa chachu ya ukombozi wa bara la Afrika kila mmoja kwa nafasi yake katika jamii ajitafakari kama anatekeleza majukumu yake kwa kuzingatia sheria, utawala bora pamoja na moyo wa uzalendo kama walivyokuwa waasisi wa taifa hili, ambao huenziwa kila mwaka.

Bendeyeko alisema ili tamasha hilo na maadhimisho ya kumbukumbu ya kuwaenzi mashujaa hao, yaweze kuwa na tija ni muhimu kwa kila mmoja kuhakikisha anaguswa na moyo wa uzalendo waliokuwa nao waasisi hao pamoja na mashujaa hao.

SHAMBA LA BHANGI LAMFIKISHA PABAYA AKAMATWA AWEKWA MAHABUSU



Na Amona Mtega,
Songea.

OSWALD Komba (61) maarufu kwa jina la Kibastola, mkazi wa kijiji cha Lipaya wilaya ya Songea mkoani Ruvuma, anashikiliwa na jeshi la polisi mkoani humo, kwa tuhuma ya kujihusisha na biashara haramu ya bhangi ambayo alishikwa na miche mingi, ikiwa imepandwa kwenye shamba ambalo inadaiwa kuwa ni la kwake lenye ukubwa wa ekari moja.

Kamanda wa polisi wa mkoa huo, Mihayo Msikhela alisema kuwa tukio hilo lilitokea Februari 20 mwaka huu majira ya mchana, huko katika kitongoji cha Kilombero kijiji cha Lipaya wilayani humo. 

Msikhela alisema kuwa baada ya kupata taarifa kutoka kwa raia wema, jeshi la polisi lilikwenda kijijini hapo na kuendesha msako mkali ndipo walipobaini shamba hilo lenye miche mingi ya bhangi, ambalo nila mtuhumiwa huyo.

Wednesday, February 25, 2015

GAUDENCE KAYOMBO UPEPO WA KISIASA WAENDELEA KUMKALIA VIBAYA MBINGA

Gaudence Kayombo, Mbunge wa Jimbo la Mbinga mkoani Ruvuma.
Na Mwandishi wetu,
Mbinga.

GAUDENCE Kayombo ambaye ni Mbunge wa jimbo la Mbinga mkoani Ruvuma, kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ameendelea kujikuta akiwa katika wakati mgumu kufuatia baadhi ya wapiga kura wake wa jimbo hilo, kuendelea kumlalamikia kwamba tokea achaguliwe katika uchaguzi mkuu uliopita hajawahi kuwatembelea kwenye maeneo yao, jambo ambalo wanakosa imani naye.

Aidha wapiga kura hao walimweleza kuwa, fedha zilizotolewa na shirika la hifadhi ya jamii (NSSF) kwa ajili ya kuwakwamua wakulima wa kahawa ambao wamejiunga kwenye vyama ushirika, hawajanufaika nazo kutokana na kulipwa bei ndogo licha ya fedha hizo kutolewa na shirika hilo kwa riba nafuu.

Walisema wanashangaa kuona malipo waliyolipwa katika msimu wa mavuno ya kahawa mwaka huu shilingi 4,500 ni kidogo, tofauti na makampuni binafsi yamekuwa yakilipa kwa bei nzuri kuanzia shilingi 4,700 hadi 5,000 kwa kilo moja ya kahawa huku yakilipa riba kubwa kwa fedha wanazokopa benki.

Tuesday, February 24, 2015

MASHINE BVR BALAA ZAKATAA KUTAMBUA WENYE VIDOLE SUGU



Na Thobias Mwanakatwe,

ZOEZI la uandikishaji wapigakura katika Daftari la Kudumu la Wapigakura limeanza katika Mkoa wa Njombe, huku likikabiliwa na changamoto nyingi, ikiwamo mashine za Biometric Voter Registration (BVR) kushindwa kutambua watu wenye vidole vyenye michilizi.

Kujitokeza kwa kasoro hizo kumekuja siku tatu tangu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, alipoeleza kuwa amenasa nyaraka zinazoonyesha Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec), ilishauriwa na mtaalam kutoka Marekani kwamba Tanzania haijawa tayari kwa teknolojia ya BVR.

Mwenyekiti wa Nec, Jaji mstaafu Damian Lubuva, akizungumza na NIPASHE alisema zoezi la uandikishaji limeanza katika mkoa wa Njombe na kwamba viongozi wa tume hiyo wapo kwa ajili ya kusimamia kuhakikisha kunakuwa na mafanikio.

Jaji Lubuva alipoulizwa kama tume imeanza na BVR ngapi, alisema suala hilo hawezi kulijibu. Hivi karibuni kuriripotiwa kuwa Nec imepata BVR 250 tu kati ya 8,000 zinazotakiwa.

CRDB YAIKOPESHA SERIKALI BILIONI 15 KULIPA MADENI YA WAKULIMA



Na Mwandishi wetu,
Iringa.

SERIKALI imepata mkopo wa Sh. bilioni 15 kulipa madeni ya mazao ya nafaka ambayo wakulima wanaidai kupitia Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA).

Waziri Mkuu,  Mizengo Pinda, alisema hayo wakati akizungumza na wananchi wa Mkoa wa Iringa akiwa kwenye ziara ya kikazi ya kukagua maendeleo mkoani humo.

Akizungumza baada ya kukagua Chama cha Ushirika cha Akiba na Mikopo (SACCOS) cha Mazombe, kilichopo Ilula, wilaya ya Kilolo, mwishoni mwa wiki iliyopita, Pinda alisema katika kipindi cha mwezi huu, serikali imepata mkopo huo kutoka Benki ya CRDB na kusambazwa kwenye mikoa mbalimbali ili kuwalipa wakulima hao.

Alisema hadi kufikia Machi, mwaka huu, serikali itahakikisha inamaliza kulipa madeni kwa wakulima waliouza mazao yao kwa NFRA.

MFUKO WA KOROSHO WAPONGEZWA KWA JITIHADA YA KUENDELEZA ZAO HILO

Mwenyekiti wa mfuko wa kuendeleza zao la korosho Tanzania (WAKFU) Athuman Nkinde, akizungumza na wakulima wa kijiji cha Litumbakuhamba kata ya Lituhi (hawapo pichani) wilayani Nyasa mkoa wa Ruvuma, ambapo alikuwa akiwahamasisha kuzalisha zao hilo kwa wingi ili kuweza kuondokana na umasikini.
Na Kassian Nyandindi,

Nyasa.

MWENYEKITI wa Halmashauri wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma, Oddo Mwisho amepongeza jitihada zinazofanywa na Mfuko wa kuendeleza zao hilo Tanzania (WAKFU) kwa kuwapatia mikorosho mipya wananchi wake, ili waweze kuzalisha zao hilo kwa wingi na kuinua uchumi wa wilaya hiyo.

Aidha Mwenyekiti huyo amewataka wakulima wa zao hilo wilayani humo, kuhamasisha wakulima wenzao kushiriki kikamilifu, katika uzalishaji wa zao hilo jambo ambalo litawafanya waweze kuwa na kipato ikiwemo pia kuondokana na umasikini.  

Mwisho alisema hayo alipokuwa mgeni rasmi kwenye mkutano wa kuhamasisha upandaji wa miche bora ya korosho, uliofanyika katika kijiji cha Litumba kuhamba kata ya Lituhi wilayani humo, ambao ulihudhuriwa na baadhi ya viongozi wa mfuko wa kuendeleza zao hilo hapa nchini.

“Ndugu zangu wakulima, ninyi ndio mabalozi wakuhamasisha wananchi wenzenu wazalishe zao hili kwa wingi kwa maendeleo ya wilaya yetu, tunapotoka hapa tuondoke na sura mpya kila mmoja ajifikirie kuweka jitihada katika uzalishaji wa zao hili, kwa manufaa ya sasa na baadaye”, alisema Mwisho.

SISTA WA KANISA KATOLIKI JIMBO LA IRINGA AFARIKI DUNIA, SITA WAJERUHIWA VIBAYA



Na Kassian Nyandindi,
Songea.

SISTA Innocensia Kisaka (33) wa kanisa Katoliki, Jimbo la Iringa mkoani Iringa amefariki dunia na wenzake sita kujeruhiwa vibaya baada ya gari walilokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na gari jingine, ambalo lilikuwa mbele yao katika kijiji cha Sanangura, Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma.

Ajali hiyo ilitokea kwenye barabara ya kutoka Njombe kwenda Songea, ambapo Kamanda wa Polisi wa mkoa huo, Mihayo Msikhela alisema tukio hilo lilitokea Februari 20 mwaka huu majira ya usiku, huku akimtaja aliyefariki dunia kuwa ni Sista huyo wa kanisa Katoliki.

Kadhalika Msikhela aliwataja waliojeruhiwa ambao hivi sasa, wamelazwa katika Hospitali ya misheni Peramiho mkoani humo kuwa ni; Padre Jastine Sapila (70), Sista Christine Banda (63) Sista Karomere Mfuse (48) Erasto (20) Karo Mhagama (21) na Thadei Charles (20) wote wakazi wa Seminari kuu Peramiho.

Sunday, February 22, 2015

WAKUU WA WILAYA WATEULE WATAKA USHIRIKIANO WASEMA WAPO TAYARI KUCHAPA KAZI

Rais Jakaya Kikwete.

Na Mwandishi wetu,
Tunduru.

WAKUU wa wilaya wateule, ambao wanakwenda kuchukua nafasi ya mkuu wa wilaya ya  Mbozi, Ahamad Namohe na Mariam Jumaa aliyepangiwa kwenda wilaya ya  Lushoto, kwa nyakati tofauti wamewataka wananchi wa wilaya hizo kutoa ushirikiano wa kutosha kwao, ili waweze kusimamia kikamilifu shughuli za kimaendeleo wakati watakapokuwa katika maeneo hayo. 

Sambamba na maelezo hayo, pia wateule hao walisema watazingatia wanatekeleza majukumu yao ya kazi kwa kuhakikisha hawata muangusha, Rais Jakaya kikwete ambaye aliwateua katika kutekeleza na kusimamia maendeleo ya wananchi wake hususani kwenye nyanja ya elimu, afya na maji na mambo mengine mengi huko waendako.

Aidha katika mahojiano hayo, walitumia nafasi hiyo kumpongeza Rais huyo kwa kuwaona na kuwaamini kuwa wanao uwezo, wa kuitumikia nchi yao.

KIKONGWE ALIYEKATWA NYETI TUNDURU APATIWA MATIBABU HOSPITALI

Na Steven Augustino,

Tunduru.

KIKONGWE mwenye umri wa miaka 70, ambaye ni mkazi wa kijiji cha Majimaji wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma, Patrick Vitus amelazwa katika hospitali ya wilaya hiyo, akiwa amepoteza fahamu (hajitambui) baada ya kukatwa sehemu zake za siri.

Taarifa za tukio hilo zinaeleza kuwa, babu huyo alifanyiwa kitendo hicho na mkwe wake aliyefahamika kwa jina la Zainabu Said.

Mjomba wa majeruhi huyo, Mussa Said akizungumzia juu ya kitendo hicho alisema, kilitokea majira ya usiku wa kuamkia Februari 20 mwaka huu.

Alisema wakati linafanyika hilo, yeye alikuwa akitokea katika mazingira ya msitu ambao upo jirani na mashamba yaliyopo katika kitongoji kipya cha Lukumbule, kilichopo kata mpya ya Majimaji wilayani humo.

USHIRIKA NAMTUMBO YASAMBAZA WALIMU MASHULENI KUANZA MAZOEZI YA KUFUNDISHA



Na  Yeremias Ngerangera,
Namtumbo.

CHUO cha ualimu, Ushirika wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma, kimesambaza wanachuo kutoka katika chuo hicho kwenda shule mbalimbali za msingi wilayani humo, ili waweze kuanza mazoezi ya kufundisha watoto shuleni.

Mwandishi wetu akizungumza na Mkuu wa chuo hicho, Awadh Nchimbi alisema kuwa tayari wanachuo 120 wamekwisha pelekwa katika shule hizo, wakiwemo wanaume 80 na wanawake 40.

Alifafanua kuwa, chuo kimedhamiria kufanya hivyo ili kuweza kujenga misingi imara ya kuwajengea uwezo wa kufundisha wanachuo hao pale wanapokuwa darasani, ili baadaye watakapohitimu masomo yao waweze kufanya vyema kwa vitendo na kufuata weledi wa kazi ya ualimu.

HAKIMU MAHAKAMA YA MWANZO SONGEA ABURUTWA MAHAKAMANI NA TAKUKURU

Yustina Chagaka, Mkuu wa TAKUKURU mkoani Ruvuma.


Na Kassian Nyandindi,
Songea.

HAKIMU wa Mahakama ya Mwanzo, Deusdedith Malembo na Michael Haulle aliyekuwa askari wa kituo kikuu cha Polisi Songea mjini mkoani Ruvuma, wote kwa pamoja wameburutwa katika Mahakama ya mkoa huo, kwa kosa la kuomba na kupokea rushwa.
 
Watuhumiwa hao wamefikishwa katika mahakama hiyo, baada ya kufunguliwa kesi ya jinai namba 15/2015 huku ikiendeshwa na mwendesha mashitaka wa TAKUKURU, Herman Malima mbele ya Hakimu, Simon Kobelo.

WATUMIAJI WA ARV WATAKIWA KUFUATA MAELEKEZO YA WATAALAMU



Na Amon Mtega,
Songea.

WATU wanaotumia dawa za kurefusha maisha (ARV) mkoani Ruvuma, wametakiwa kufuata maelekezo ya watalaamu wao, namna ya kutumia dawa hizo na kuachana na maelekezo yanayotolewa na watu wengine mitaani, ili waweze kuepukana na madhara yanayoweza kutokea baadaye.   

Wito huo ulitolewa na Mratibu wa magonjwa ya kifua kikuu na UKIMWI, wilaya ya Songea mkoani humo, Adam Ngunga kwenye mafunzo elekezi kwa wanachama zaidi ya 80 kutoka sehemu mbalimbali mkoani Ruvuma, wa shirika lisilokuwa la kiserikali (DMI) yaliyofanyika mjini hapa.

Wanachama hao walielekezwa namna ya kuepukana na maambukizi ya ugonjwa huo, pamoja na matumizi ya dawa za ARV kwa mgonjwa ambaye tayari anastahili kutumia dawa hizo, mara baada ya kushuka kwa  kinga zake mwilini.

SONAMCU WAGOMEA MKUTANO BAADA YA KUKOSA POSHO



Na Nathan Mtega,
Songea.

MKUTANO Mkuu maalumu wa Chama cha ushirika cha wakulima wa tumbaku Songea na Namtumbo, mkoani Ruvuma (SONAMCU) uliopangwa kufanyika Februari 18 mwaka huu umeshindwa kufanyika, baada ya Wajumbe wa mkutano huo kugoma baada ya kuambiwa na uongozi wa juu wa chama hicho kwamba,  hakuna fedha ya posho kwa ajili ya kujikimu siku mkutano huo ulipotakiwa kufanyika.

Hatua hiyo ya wajumbe wa mkutano huo kugomea, ilianza baada ya kutokea kwa mvutano miongoni mwao na uongozi wa juu wa chama hicho mjini hapa, pamoja na Meneja wa SONAMCU,  Christopther Ugulumo ambaye alitoa taarifa kwa wajumbe kuwa mkutano huo hautakuwa na posho na yeye hakuitisha bali umeitishwa na mrajisi wa vyama vya ushirika mkoani humo.

Baada ya kauli hiyo, ndipo wajumbe wa mkutano huo walipoanza kueleza kuhusu msimamo wao wa kutoshiriki katika mkutano mpaka suala la malipo ya posho stahiki yatapowekwa wazi, na kwamba wakati malumbano hayo yakiendelea kwa muda wa zaidi ya dakika 45 ndipo mrajisi msaidizi alishauri kupigwa kura ili kujua wanaokubali mkutano ufanyike na posho zitalipwa baada ya fedha kupatikana, na wanaokataa kufanyika kwa mkutano mkuu wa uchaguzi.

AKATWA SEHEMU ZA SIRI HUKU ZIKIACHWA ZINABEMBEA



Na Amon Mtega,
Tunduru.

MKAZI mmoja wa kijiji cha Majimaji, wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma, Patrick Vitus (70) amekatwa sehemu zake za siri na kuziacha zikiwa zinabembea na mtu aliyefahamika kwa jina la Zainabu Said (32) ambaye anadaiwa kuwa ni mpwa wake, baada ya kumkatalia kwenda kumfuata mme wa Zainabu aliyekuwa kwa mke mdogo.

Akizungumza na kwa njia ya simu Afisa mtendaji wa kijiji hicho, Hussein Mkali alisema kuwa tukio hilo lilitokea February 20 mwaka huu majira ya usiku katika maeneo ya mashamba ya kijiji hicho, ambako walikuwa wakifanya shughuli za kilimo.

Mkali alisema kuwa Vitus alikatwa nyeti hizo na kuziacha zikiwa zinabembea baada ya kumkatalia Zainabu, kumpeleka kwa mme wake ambaye alidaiwa kuwa alikuwa kwa mke mdogo ambaye ni mke wake. 

MKUU WA KITUO CHA POLISI AHUKUMIWA KWENDA JELA KWA KUMBAKA MAHABUSU



Na Mwandishi wetu,
Njombe.

MAHAKAMA ya Hakimu mkazi mkoa wa Njombe, imemhukumu aliyekuwa mkuu wa kituo cha Polisi Ilembula kifungo cha miaka 30 jela, baada ya kukutwa na hatia ya kumbaka  mtuhumiwa aliyekuwa ndani ya mahabusu.

Hukumu hiyo ilitolewa na Hakimu Augustine Rwezile, baada ya mshtakiwa huyo James Nyambenga kukiri kosa hilo mahakamani, ambapo mshakiwa huyo anadaiwa kumtoa msichana huyo kwenye chumba cha mahabusu, alikokuwa anashikiliwa na kumbaka.

Mwanamke huyo ambae ni mhudumu wa bar, alikuwa anashikiliwa kwenye mahabusu ya kituo hicho kwa tuhuma za uzurulaji.

Akisoma hukumu hiyo Hakimu, Rwezile alisema ushahidi uliotolewa na upande wa mlalamikaji na vielelezo vya daktari aliyempima msichana huyo viliweza kuithibitishia Mahakama kuwa, mtuhumiwa alitenda kosa hilo.

Chanzo: Gazeti la Nipashe.

Thursday, February 19, 2015

OFISA UTUMISHI MBINGA ANA MATATIZO NI VYEMA HATUA STAHIKI ZICHUKULIWE SASA


Waziri wa nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa; Hawa Ghasia.

Na Kassian Nyandindi,

Mbinga.

KWA nyakati tofauti baadhi ya watumishi ambao ni Watendaji wa vijiji na kata, wilayani Mbinga mkoa wa Ruvuma, wameendelea kumshutumu Ofisa utumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma, Emmanuel Kapinga kuwa amekuwa akifanya upendeleo wakati wa upandishaji vyeo kwa watumishi wa kada hizo, jambo ambalo wamedai kuwa kwa namna moja au nyingine, huenda kuna mkono mchafu wa rushwa.

Aidha wameiomba Taasisi ya Kuzuia, Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) na vyombo vingine vinavyotetea watumishi kazini, kufanya upembuzi yakinifu ikiwemo kuchunguza mwenendo wa utendaji kazi wa Ofisa huyo, ili kuondoa matatizo yanayoendelea kujitokeza mara kwa mara katika ofisi hiyo na ambayo yanawafanya wakose haki zao za msingi.

Mwandishi wetu, amebaini pia hata utekelezaji wa Waraka wa maendeleo ya utumishi namba moja wa mwaka 2013 ambao unawataka watendaji wakuu katika halmashauri nchini, kutekeleza majukumu yao ipasavyo kwa kuwapandisha vyeo watumishi wa kada hizo, amekuwa hatekelezi kwa wakati huku agizo hilo tangu lilipotolewa  na Ofisi ya Rais, chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), ndio maana leo linazua malalamiko miongoni mwao.

Pia waraka ulitolewa na Menejimenti ya utumishi wa umma, Februari 27 mwaka 2014 umeagiza na kutaka kutumika kwa miundombinu husika ya utumishi kazini, na kuondoa changamoto mbalimbali zilizokuwa zikijitokeza katika utekelezaji wake hasa kutokana na uhaba wa watumishi wenye sifa zinazotakiwa, katika usimamizi wa rasilimali na miradi ya maendeleo katika ngazi ya kijiji, mtaa na kata.

Wednesday, February 18, 2015

JENISTA: HAMASISHENI WANANCHI WAJIANDIKISHE KATIKA DAFTARI LA WAPIGA KURA

Jenista Mhagama.


Na Kassian Nyandindi,
Songea.

WAZIRI wa nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge, Jenista Mhagama amewataka viongozi wa Jumuiya ya wazazi, vijana na umoja wa wanawake Tanzania (UWT) kuhakikisha wanafanya kazi ya kuhamasisha wananchi, kwenda kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura na kuipigia kura katiba pendekezwa, ili kutoa fursa ya upigaji kura kwa wananchi  wengi hasa katika kipindi cha uchaguzi mkuu ujao.

Jenista ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Peramiho, kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) alitoa wito huo, wakati alipokuwa kwenye hafla fupi ya kupongezwa kwake kuwa katika nafasi hiyo ya uwaziri, iliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa parokia ya  Bombambili, Manispaa ya Songea  mkoani Ruvuma.

Hafla hiyo ilihudhuriwa na viongozi wote wa jumuiya za CCM, ambapo alisema pamoja na mambo yote ya maendeleo ambayo yanafanywa na serikali, kazi iliyobaki katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu ni kuhakikisha wananchi wanajiandikisha kwenye daftari la kupigia kura, pamoja na kuipigia kura katiba pendekezwa.

UTEUZI WA WAKUU WA WILAYA WAPYA NA WALE WANAOBAKIA KATIKA VITUO VYAO VYA KAZI HUU HAPA



JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA WAZIRI MKUU
Anuani ya Simu: WAZIRI MKUU
Simu Nambari: 026 2322904
e-mail: pm@pmo.go.tz
S.L.P 980
DODOMA

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI:

Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, amefanya mabadiliko ya Wakuu wa Wilaya ili kuboresha utendaji kazi. Mabadiliko hayo yamezingatia kuwepo kwa nafasi wazi ishirini na saba (27) zilizotokana na:

a) Kufariki dunia Wakuu wa Wilaya 3;
b) Kupandishwa cheo Wakuu wa Wilaya 5 kuwa Wakuu wa Mikoa;
c) Kupangiwa majukumu mengine Wakuu wa Wilaya 7; na
d) Kutengua uteuzi wa Wakuu wa Wilaya 12.

Katika mabadiliko hayo, Mheshimiwa Rais amewateua Wakuu wapya wa Wilaya 27 ili kujaza nafasi hizo wazi.
Aidha, Wakuu wa Wilaya sitini na nne (64) wamebadilishwa vituo vya kazi na Wakuu wa Wilaya arobaini na mbili (42) wameendelea kubaki katika vituo vya sasa.

1) Wakuu wa Wilaya waliofariki dunia

JINA NA WILAYA

1. Capt. (mst) James C. Yamungu Serengeti
2. Anna J. Magoha Urambo
3 Moshi M. Chang’a Kalambo

2) Wakuu wa Wilaya waliopandishwa cheo

Wakuu wa Wilaya wafuatao wamepandishwa cheo kuwa Wakuu
wa Mikoa

JINA WILAYA MKOA ALIOPANGIWA

1. John Vianney Mongela Arusha Kagera
2. Amina Juma Masenza Ilemela Iringa
3. Dkt. Ibrahim Hamis Msengi Moshi Katavi
4. Halima Omari Dendego Tanga Mtwara
5. Daudi Felix Ntibenda Karatu Arusha

3) Wakuu wa Wilaya waliopangiwa majukumu mengine

Wakuu wa Wilaya ambao uteuzi wao umetenguliwa na
watapangiwa kazi nyingine ni hawa wafuatao;

JINA NA WILAYA

1. Brig. General Cosmas Kayombo Simanjiro
2. Col. Ngemela Elson Lubinga Mlele
3. Juma Solomon Madaha Ludewa
4. Mercy Emanuel Silla Mkuranga
5. Ahmed Ramadhan Kipozi Bagamoyo
6. Mrisho Gambo Korogwe
7. Elinas Anael Pallangyo Rombo

4) Wakuu wa Wilaya Wanaotenguliwa

Wakuu wa Wilaya ambao uteuzi wao umetenguliwa kutokana na
sababu za umri, kiafya na nyinginezo na vituo vyao ni kama
inavyoonekana hapa chini:

JINA NA WILAYA

1. James Kisota Ole Millya Longido
2. Elias Wawa Lali Ngorongoro
3. Alfred Ernest Msovella Kongwa
4. Dany Beatus Makanga Kasulu
5. Fatma Losindilo Kimario Kisarawe
6. Elibariki Emanuel Kingu Igunga
7. Dr. Leticia Moses Warioba Iringa
8. Evarista Njilokiro Kalalu Mufindi
9. Abihudi Msimedi Saideya Momba
10. Martha Jachi Umbula Kiteto
11. Khalid Juma Mandia Babati
12. Eliasi Goroi Boe Boe Goroi Rorya

5) Wakuu wa Wilaya wapya walioteuliwa