Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa. |
Songea.
MADIWANI katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea mkoani
Ruvuma, wametakiwa kuachana na makundi yanayoigawa Manispaa hiyo kwani endapo
wakiendelea kufanya hivyo wamekuwa wakikwamisha utekelezaji wa miradi ya
maendeleo ya wananchi.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alisema hayo jana wakati alipokuwa
kwenye ziara yake ya siku moja katika mkoa huo.
Majaliwa alisema hayo alipokuwa akizungumza na watumishi
pamoja na Madiwani hao mjini hapa, ambapo aliwaambia endapo kama watashindwa kumaliza
tofauti zao yeye atawafukuza.
“Madiwani mnaigawa halmashauri, pamoja na nguvu mliyonayo ya
kuiendesha halmashauri lakini mnaiendesha vibaya, miradi haijengwi vizuri mmeingiza
maslahi yenu binafsi wakati mwingine pesa zinatumwa mnaanza kubishana tu, sasa
ni mwisho mkiendelea tutawafukuza, alisema Majaliwa.
Alibainisha kuwa Serikali inakusanya kodi ili wananchi waweze
kupata maendeleo lakini wao wanachelewesha miradi ya maendeleo kwa malengo ya
kuikwamisha Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) hivyo hatakubali na atawafukuza.
Hata hivyo alimpongeza Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Tina
Sekambo kwa kazi nzuri anayoifanya na kumtaka kuripoti kwake endapo pesa zitaingia
kisha Madiwani kuanza kubishana bila utekelezaji ili awashughulikie hata kama atakuwa
ni Meya wa Manispaa hiyo.
No comments:
Post a Comment