Tunduru.
KIJIJI cha Mindu kilichopo katika kata ya Mindu Wilayani Tunduru mkoa wa Ruvuma wakazi wake wanaoishi katika kijiji hicho wameondokana na shida ya upatikanaji wa maji safi na salama, baada ya uongozi wa Kanisa la Anglikana jimbo la Masasi kuwajengea kisima kikubwa cha maji.
KIJIJI cha Mindu kilichopo katika kata ya Mindu Wilayani Tunduru mkoa wa Ruvuma wakazi wake wanaoishi katika kijiji hicho wameondokana na shida ya upatikanaji wa maji safi na salama, baada ya uongozi wa Kanisa la Anglikana jimbo la Masasi kuwajengea kisima kikubwa cha maji.
Imeelezwa kuwa ujenzi wa kisima hicho,
Kanisa lilitekeleza mradi huo kupitia mradi wa Uboreshaji wa afya ya mama na
mtoto (CHIP).
Wakizungumza baada ya kuzinduliwa
ujenzi wa kisima hicho, baadhi ya wanawake wa kijiji hicho mbali na kupongeza
juhudi zilizofanywa na uongozi husika walisema hivi sasa hata ndoa zao nyumbani
wanakoishi kijijini humo zitakuwa salama kwa kuwa hawataweza kutumia muda mrefu
kutafuta huduma ya maji mbali na makazi yao.
Debora Mambo na Joyce Daud kwa
nyakati tofauti walisema kuwa awali ilikuwa ikiwalazimu kutoka majumbani mwao
majira ya saa nane usiku na kurudi majira ya saa 11 alfajiri wakitoka
kutafuta maji kwa ajili ya matumizi mbalimbali nyumbani jambo ambalo lilikuwa
likisababisha migogoro mingi kwenye ndoa zao.
Walisema maisha ya wananchi wa kijiji
hicho hasa wanawake yalikuwa magumu kutokana na ukosefu wa huduma hiyo kwa
sababu wakati mwingine walikuwa wakikosa hata nafasi ya kufanya shughuli zao za
maendeleo.
Kwa upande wake Mratibu wa CHIP,
Geofrey Monyesa amewashukuru watumishi wa halmshauri ya wilaya ya Tunduru kwa
ushirikiano mkubwa walioutoa katika kufanya utafiti wa ujenzi wa mradi huo na
hatimaye kufanikiwa kuchimba kisima ambacho sasa kitawaondolea kero ya maji
iliyodumu kwa muda mrefu katika kijiji hicho.
Alisema mradi wa kisima cha maji katika
kijiji cha Mindu ni kati ya miradi 24 ya visima vya maji vilivyotekelezwa katika
wilaya ya Masasi ambayo imepata kisima kimoja na Tunduru visima 23 ambapo lengo
lake ni kuwapunguzia wasichana waliopo shuleni na wanawake majumbani kutembea
umbali mrefu kutafuta huduma hiyo.
Monyesa alifafanua kuwa kukamilika
kwa miradi hiyo ambayo inatekelezwa na Kanisa la Anglikana jimbo la Masasi, itasaidia
wanafunzi wa kike kupata muda mwingi wa kuhudhuria masomo darasani na muda wa
kujisomea pale wanaporudi nyumbani.
Naye Kaimu Mkurugenzi mtendaji wa
halmashauri ya wilaya ya Tunduru Chiza Malando aliongeza kuwa kufunguliwa kwa
kisima cha maji ni kati ya juhudi kubwa zinazofanywa na Serikali ya awamu ya
tano kwa kushirikiana na wafadhili wa ndani na nje ya nchi katika mkakati wake
kuboresha maisha ya Watanzania.
Aliwataka wananchi kuendelea kuunga
mkono juhudi mbalimbali zinazofanywa na wafadhili pamoja na Serikali yao
ambayo imedhamiria kuwatoa katika adui wa maradhi, umaskini na ujinga huku akisisitiza
kuwa mpango wa Serikali ya awamu ya tano ni kuona kila mmoja anapata maji safi
na salama.
Malando aliwaomba wananchi wa wilaya
hiyo kuendelea kutoa ushirikiano kwa Serikali yao iliyopo madarakani kwa
kufanya kazi za kujitolea kama vile ujenzi wa miundombinu ya shule, barabara, maji
na afya badala ya kuendelea kuwa walalamikaji jambo ambalo linachelewesha kukua
kwa maendeleo yao.
No comments:
Post a Comment