Dodoma.
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dokta John Pombe Magufuli, ametoa
onyo kali kwa watakaojihusisha na vitendo vya rushwa wakati wa mchakato wa
uchaguzi mkuu wa Viongozi wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) ndani ya CCM.
Hayo alisema leo mjini Dodoma wakati
akizindua mkutano wa tisa wa wa Umoja huo huku akieleza kuwa hatosita kumchukulia
hatua mtu yeyote atakayebainika kutumia mbinu za ujanja ujanja ikiwemo rushwa
ili achaguliwe.
“Nikigundua kulikuwa na ukiukwaji
katika uchaguzi huu nitachukua hatua na hili ni kwa UVCCM, UWT, Wazazi na
jumuiya nyingine, kwa sababu mimi sikupita kwa rushwa kama kuna mchezo huo
mchafu ulifanyika tutakaa na tutafuta huo uchaguzi”, alisema.
Alifafanua kuwa wamchague kiongozi
kwa kumtanguliza Mungu ambaye ataweza kuwa mtetezi wa akina mama na atakayeweza
kuthamini kanuni na katiba ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
“Haiwezekani tukawa na viongozi ambao
wametekwa na watu wengine kwa maslahi ya mambo fulani, niwaombe wanaCCM
wenzangu tunafahamu UWT iliyokuwa ya akina Sophia Simba, siyo UWT tuliyo nayo
sasa nawapenda akina mama naomba mnisaidie katika hili mtakayemchagua awe
anajitambua kwamba kuongoza ni kuwatumikia anaowaongoza.
No comments:
Post a Comment