Dokta John Magufuli. |
JOHANNESBURG, Afrika Kusini.
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Dokta John Magufuli ametunukiwa tuzo ya amani ya Mandela (Mandela
Peace Prize) kwa kuendeleza shughuli ya kulinda amani na kupigania usawa katika
kijamii.
Kamati ya tuzo za Mandela kwa mwaka
2017 ilipokea maombi ya wa wania tuzo 4,956.
Wengine waliotunukiwa ni Rais Uhuru
Kenyatta aliyeshinda tuzo ya Mandela ya Demokrasia kutokana na kuendeleza
demokrasia nchini Kenya.
Kadhalika Mahakama ya juu nchini
Kenya na Jeshi la Zimbabwe zimetunukiwa tuzo ya ujasiri (Mandela Boldness) kwa
kufanya uamuzi kwa ujasiri kwa masilahi ya mataifa yao.
Rais wa taasisi ya Mandela, Dokta
Paul Kananura alisema Rais Kenyatta ametunukiwa kwa kudhihirisha demokrasia kwa
kukubali uamuzi wa Mahakama ya juu hivyo kuheshimu kanuni za utengano wa
mamlaka husika.
Mahakama ya juu ya Kenya ilibatilisha
matokeo ya Urais katika uchaguzi wa Agosti 8 mwaka huu yaliyompatia ushindi
Kenyatta na kuamuru uchaguzi kurudiwa ambao alishiriki na kuibuka mshindi.
“Hii inaonesha kuwa Rais Kenyatta
amechangia katika uimarishaji wa demokrasia Kenya”, alisema Dokta Kananura.
Rais wa Chad, Idriss Itno naye amepata
tuzo ya Mandela ya Ulinzi (Mandela Security) kutokana na sera ya kupambana na
ugaidi katika maeneo ya Sahel na ziwa Chad.
Mwingine ni Rais wa Burundi, Pierre
Nkurunziza aliyetuzwa tuzo ya ujasiri (Mandela Courage).
No comments:
Post a Comment