Na Mwandishi wetu,
Songea.
HOJA Project ni asasi ambayo
isiyokuwa ya kiserikali yenye makao yake makuu mjini Songea, mkoani Ruvuma
inatarajia kutumia kiasi cha shilingi milioni 900 kwa ajili ya ujenzi wa
majengo mbalimbali ya chuo cha ualimu mkoani humo.
Kadhalika ujenzi wa baadhi ya majengo
ya chuo umeanza kujengwa ikiwa ni pamoja na majengo ya utawala, ukumbi, vyoo,
mabweni ya kulala wanafunzi pamoja na mabanda kwa ajili ya kufugia mifugo.
Mratibu wa COCO Tanzania ambaye ni
Meneja mkuu wa miradi ya katika sasi hiyo, Oswin Mahundi alisema hayo mjini
hapa wakati alipokuwa akizungumza na mwandishi wetu ofisini kwake.
Alisema kuwa ujenzi wa majengo hayo
utakapokamilika utaanza kutoa mafunzo mbalimbali kwa ngazi ya stashahada na
cheti katika fani ya ualimu, usimamizi wa biashara, ukarani, kompyuta, kilimo,
uhasibu, maendeleo ya jamii na masuala ya utalii.
Mahundi alieleza kuwa chuo hicho
kinatarajia kuchukua wanafunzi kuanzia mwaka 2018 ambapo aliiomba Serikali
kutoa ushirikiano na kuwataka wananchi wa mkoa huo kuchangamkia fursa hiyo
katika kujiendeleza.
Pia alifafanua kuwa Hoja inamiliki na
kuendesha shule za sekondari mbalimbali ikiwemo shule ya Hoja sekondari na
shule ya sekondari Mshangano zote zilizopo katika Manispaa ya Songea, shule ya
sekondari Kindimba juu iliyopo wilaya ya Mbinga pamoja na kituo cha elimu
kiitwacho Elimika.
Aliongeza kuwa wamekuwa
wakishirikiana na jamii na asasi zingine za kijamii kuendesha shule za
chekechea ambazo ni Olamayani nursary school iliyopo Monduli mkoani Arusha, MCODE
mkoani Kilimanjaro, MLASEO mkoani Pwani, Lupembe mkoani Njombe, Kids are kings
iliyopo Manispaa ya Songea na Litisha Songea vijijini.
Pamoja na mambo mengine, Hoja project
ilianza kama wazo mnamo mwaka 2005 chini ya mratibu huyo kwa kupitia magumu
katika safari yake ya elimu kwa nia ya kujenga shule ambazo itasaidia kusoma
bure watu wasiokuwa na uwezo wa kifedha au kwa gharama nafuu.
No comments:
Post a Comment