Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (TAMISEMI) Seleman Jafo akizungumza na waandishi wa habari leo Mkoani Dodoma juu ya kumsimamisha kazi Mkurugenzi mtendaji wa wilaya ya Nkasi, Julius Kaondo. |
Na Mwandishi wetu,
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais
(TAMISEMI) Seleman Jafo amemsimamisha kazi Mkurugenzi mtendaji Wilayani Nkasi
mkoa wa Rukwa, Julius Kaondo kwa tuhuma za rushwa na matumizi mabaya
yaliyoisababishia Serikali hasara ya shilingi bilioni 7.
Hatua hiyo ya Waziri Jafo
kumsimamisha kazi Mkurugenzi huyo alisema kuwa imefuatia baada ya kushindwa
kusimamia alichopaswa kukifanya kwa wakati katika eneo lake la utumishi.
Taarifa za kusimamishwa huko
zilielezwa leo na Waziri huyo wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa
habari Mkoani Dodoma mjini hapa.
“Natumia sheria ya Serikali za Mitaa
sura ya 4 kifungu cha kwanza hadi tano pamoja na sura ya 287 ya sheria hiyo
ambavyo vinanipa mamlaka haya”, alisema Jafo.
Jafo aliongeza kuwa fedha hizo
zilikuwa za mradi wa maji wa kijiji cha Kamwanda wilayani humo, ambako Mkurugenzi
Kaondo anadaiwa kushirikiana na mmoja wa maofisa kutoka Wizara ya maji
kuhujumu fedha za mradi huo.
No comments:
Post a Comment