Na Kassian Nyandindi,
Songea.
WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amemuagiza Afisa ardhi wa
Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma, Kundaeli Fanuel Ndemfoo afuatilie suala la
Bibi Monica Joseph Miti na wanae ambao walidhulumiwa nyumba ya urithi na
aliyekuwa mwanasheria wa Manispaa hiyo.
Alitoa agizo hilo jana katika mkutano wa
hadhara uliofanyika kwenye kata ya Mwengemshindo baada ya kupokea bango
lililoandikwa na Bibi Miti kuomba arejeshewe umiliki wa nyumba ya marehemu
muwewe.
Alipopewa nafasi ya kueleza tatizo
lake, Bibi Miti ambaye alimtaja mwanasheria huyo kwa jina moja la Mwakasungura,
alidai kuwa mwanasheria huyo alighushi hati ya nyumba na kuwatoa ndani ya
nyumba yeye na watoto wa marehemu.
Alipoulizwa na Waziri Mkuu aeleze
alipo huyo mwanasheria, Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Tina Sekambo alijibu
kwamba alishahamishiwa wilaya ya Ukerewe.
Majaliwa amemuagiza Mkurugenzi wa
Manispaa ya Songea na Afisa ardhi wa Manispaa hiyo wafuatilie suala hilo na
wampe majibu mapema iwezekanavyo.
Hata hivyo amemuomba Bibi Miti na
wanawe wafike kuonana naye Januari 3, mwakani atakapokuwa Songea kwa mapumziko
mafupi ya mwisho wa mwaka.
No comments:
Post a Comment