Sunday, December 9, 2012

ACHOMWA MOTO NA KUFARIKI DUNIA BAADA YA KUIBA SIMU

 






Picha ya marahemu aliyeiba simu na mwili wake kuchomwa moto na kutupwa porini kijiji cha Mbesa wilayani Tunduru.(Picha na Steven Augustino)










Na Steven Augustino,
Tunduru.

Mkazi wa Kijiji cha Mbesa wilayani Tunduru mkoa wa Ruvuma, aliyejulikana kwa jina la Seif Jaffari(18) ameuawa kikatili na wananchi wenye hasira kali baada ya kumtuhumu ameiba simu.

Mauaji hayo ya kinyama yalifuatia na kipigo kikali alichokipata na wananchi hao walimchoma moto na mwili wake kuteketezwa kwa porini.

Mashuhuda wa tukio hilo walisema kuwa kabla ya kifo hicho marehemu akiwa na wenzake waliiba simu 6 ambazo zilikuwa zikichajiwa katika nyumba ya Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Chikomo aliyefahamika kwa jina moja la Mwl. Komba iliyopo kijijini humo.


Walisema baada ya kufanikisha wizi huo marehemu na wenzake waliondoka kurejea Mbesa, eneo ambalo alikutwa na wahanga watukio hilo wakati wakimtafuta.

Baada ya kundi hilo la watu waliokuwa wakimtafuta kumkuta kijijini hapo marehemu alianza kuwakimbia, baada ya kuwaona hali ambayo iliwafanya wapige kelele za kuomba msaada kwa watu wengine.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Ruvuma Deusdedith Nsemeki mbali na kuthibitisha kuwepo kwa tukio hilo alisema kuwa polisi wanaendelea kuchunguza chanzo cha tukio hilo.

Aidha kamanda Nsemeki, alikemea tabia za wananchi hao wanaotumia mwamvuli wa hasira kuchukua maamuzi ya kuua na kuwataka wananchi waache mara moja, badala yake watuhumiwa wafikishwe kwenye vyombo vya sheria.














 













   



No comments: