Thursday, December 20, 2012

AKUTWA NA MAUTI BAADA YA KUIBA MATITA YA NYASI


Na Steven Augustino,
Tunduru.

MKAZI  wa kijiji cha Tingunya  wilayani Tunduru Ruvuma, anayefahamika kwa jina la Matatizo Mohamedi(27) anashikiliwa na Jeshi la polisi kwa tuhuma za mauaji ya kukusudia katika tukio lililotokea kijijini hapo Desemba 12 mwaka huu.

Kamanda wa polisi wa mkoa huo Deusidedith Nsemeki alisema

kuwa mtuhumiwa huyo  anashikiliwa kwa tuhuma za kumuua kwa kumpiga kichwani kwa kutumia mguu(Tendegu) la kitanda baada ya kutokea ugomvi kati yao.

Kamanda Nsemeki alimtaja aliyefariki dunia katika
  tukio hilo kuwa ni mtu aliyefahamika kwa jina la Maulio Tikiri(14) aliyedaiwa kupigwa na Tendegu hilo Kichwani, na kupoteza maisha muda mfupi baada ya kufikishwa katika kituo cha afya cha Nakapanya kwa matibabu wilayani Tunduru.


Alifafanua kwamba taarifa za uchunguzi wa awali zinaonesha kuwa chanzo cha ugomvi huo kilitokana na maerehemu kutuhumiwa kuiba matita ya Nyasi, ambayo yalihifadhiwa katika eneo moja kwa ajili ya kuezekea nyumba zao.
 

Alisema mtuhumiwa huyo atafikishwa mahakamani baada ya taratibu za upelelezi kukamilika ili sheria iweze kufuata mkondo wake.
 

Akizungumzia tukio hilo mganga aliyeufanyia uchunguzi mwili wa
marehemu Tikiri Dokta Jeshi Daraja alisema kuwa chanzo cha kifo hicho ni kutokwa na damu nyingi  lulikosababishwa na kupasuka kwa fuvu la kichwa.

No comments: