Wednesday, December 5, 2012

ATEKETEZWA KWA MOTO AKITUHUMIWA KUIBA SIMU


Na Steven Augustino,
Tunduru.

MKAZI mmoja wa kijiji cha Mbesa wilayani Tunduru, mkoani Ruvuma ameuwawa kikatili, na wananchi wenye hasira kali na mwili wake kuuteketeza kwa kuchomwa moto.

Aliyefanyiwa kitendo hicho cha kinyama ni Seif Jafari(18) baada ya kumtuhumu ameiba simu.
Kabla ya mauaji hayo wananchi hao walimuangushia kipigo kikali  na kwamba
akiwa na wenzake wanadaiwa kuiba simu 6 ambazo zilikuwa zikichajiwa katika nyumba ya mwalimu mkuu wa shule ya msingi Chikomo aliyefahamika kwa jina moja la Mwl. Komba.

Walisema baada ya kufanikisha wizi huo marehemu na wenzake waliondoka na kurejea Mbesa eneo ambalo alikutwa na wahanga watukio hilo wakati wakimtafuta.
Walisema baada ya kundi hilo la watu waliokuwa wakimtafuta kumkuta kijijini hapo, marehemu alianza kuwakimbia baada ya kuwaona hali ambayo
iliwafanya wapige kelele za kuomba msaada kwa watu wengine.
Akizungumzia tukio hilo Kamanda wa polisi wa mkoa wa Ruvuma, Deusdedit Nsemeki alisema polisi wanaendelea kuchunguza chanzo cha tukio hilo.
Aidha Nsemeki alikemea tabia za wananchi hao kuchukua sheria mkononi na kufanya mauaji, na kuwataka wasifanye hivyo badala yake watoe taarifa katika vyombo vya ulinzi ili hatua za kisheria ziweze kufuata mkondo wake.

No comments: