Sunday, December 9, 2012

MADINI YA URANI NAMTUMBO BADO HAYAJAANZA KUCHIMBWA WATANZANIA TUSIPOTOSHWE

Madini ya Urani yakionekana kujitokeza juu ya ardhi katika eneo la mto Mkuju hifadhi ya Selous, wilayani Namtumbo.(Picha na Kassian Nyandindi)
Na Kassian Nyandindi,
Namtumbo.

UVUMI na kauli zilizokuwa zikielezwa na watu mbalimbali kwamba kazi ya uchimbaji wa madini aina ya Urani katika mto Mkuju uliopo pori la hifadhi ya Selous, wilayani Namtumbo mkoani Ruvuma kwamba umeanza sio kweli, badala yake kinachofanyika ni kukamilisha kazi ya utafiti wa madini hayo.

Waandishi wa habari wa wa mkoa huo wamefanya ziara maalumu ya kutembelea mradi wa mto huo ambako kampuni ya Mantra Tanzania inatarajia kuanza ujenzi wa mgodi wa madini hayo.

Kauli zinazotolewa na watu mbalimbali ambapo wamekua wakidai mradi huo haufai kwa kuwa unahatarisha maisha ya binadamu kutokana na athari za mionzi na uharibifu wa mazingira.


Ilikuwa ni ziara ya kikazi zaidi iliyowapa fursa waandishi wa habari wote wa Ruvuma kuingia ndani ya Pori la hifadhi ya Selous, na katika maeneo ambako utafiti umethibisha uwepo wa latili milioni 119 za madini ya Urani, zitakazochimbwa kwa miaka 12 baada ya uwekezaji wa dola bilioni moja za Marekani, utakaoiwezesha Tanzania kuweka kibindoni mapato ya dola milioni 640.

Kwa sehemu kubwa wanaharakati kutoka mashirika mbalimbali wamekuwa wakidai kwamba mradi huo ni hatari kwa binadamu na mazingira.

Kilichopo sasa wataalamu wa kampuni ya Mantra Tanzania, wamekuwa wakitoa elimu kwa wananchi juu ya suala la utunzaji wa mazingira na athari za madini hayo, kabla ya kazi ya uchimbaji kuanza wakati wakisubiri kibali kutoka serikalini.

 

No comments: