Thursday, April 12, 2018

DOKTA MAGUFULI AMBADILISHA MPAMBE WAKE WENGINE WAPANDISHWA VYEO


Na Mwandishi wetu,

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta John Pombe Magufuli, ameridhia kuwapandisha vyeo maofisa 28 wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) kuanzia leo Aprili 12 mwaka huu.

Tukio hilo limeenda sambamba huku akimbadilisha Msaidizi wake Kanali Mbaraka Mkeremy, ambaye amempandisha cheo na atapangiwa kazi nyingine jeshini.

Kadhalika Rais Magufuli amekukubali kumpandisha cheo kutoka Luteni Kanali kuwa kanali D.P.M Murunga na kuwa mpambe wa Rais akichukua nafasi ya Kanali Mkeremy.


Vilevile akitoa taarifa ya uteuzi huo, Mkuu wa Majeshi Jenelari Venancy Mabeyo alisema kuwa maofisa walioteuliwa wanakwenda kuimarisha safu za utendaji kazi kijeshi na kwamba maofisa wote hao, watavalishwa vyeo vyao Aprili 13 mwaka huu katika makao makuu ya Jeshi Upanga jijini Dar es salaam.

Katika uteuzi huo amewapandisha vyeo pia maofisa wa ngazi mbalimbali Jeshini ikiwa ni pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe Mkoani Kigoma, Kanali M E Gaguti ambaye sasa anapanda cheo na kuwa Brigedia Jenelari na kurejeshwa jeshini.

No comments: