Wednesday, April 18, 2018

DOKTA MAGUFULI ATOA MKONO WA POLE KWA FAMILIA YA MRISHO GAMBO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta John Pombe Magufuli akiwasili mtaa wa Muheza Kariakoo jijini Dar es salaam, kutoa pole kwa familia ya Mzee Mashaka Gambo kwa kufiwa na mkewe ambaye pia ni mama mzazi wa  Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo kwa kufiwa na mama yake mzazi Marehemu Rehema Paul Mumbuli leo Aprili 18 mwaka huu.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta John Pombe Magufuli akiweka saini kwenye kitabu cha maombolezo baada ya kuwasili mtaa wa Muheza Kariakoo jijini Dar es salaam, kutoa pole kwa familia ya Mzee Mashaka Gambo kwa kufiwa na mkewe ambaye pia ni mama mzazi wa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta John Pombe Magufuli akimpa pole Mzee Mashaka Gambo kwa kufiwa na mkewe Marehemu Rehema Paul Mumbuli leo Aprili 18 mwaka huu.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta John Pombe Magufuli akimpa pole Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo alipowasili nyumbani kwao mtaa wa Muheza Kariakoo jijini Dar es salaam kumfariji kwa kufiwa na mama yake mzazi Marehemu Rehema Paul Mumbuli leo Aprili 18 mwaka huu.
 Mama Janeth Magufuli akimpa pole  Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo alipofika nyumbani kwao mtaa wa Muheza Kariakoo jijini Dar es salaam kumfariji kwa kufiwa na mama yake mzazi Marehemu Rehema Paul Mumbuli.
 Mama Janeth Magufuli akimpa pole Mzee Mashaka Gumbo kwa kufiwa na mkewe ambaye pia ni mama mzazi wa  Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo alipofika nyumbani kwao mtaa wa Muheza Kariakoo jijini Dar es salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta John Pombe Magufuli akiaga waombolezaji, baada ya kutoa mkono wa pole kwa familia ya Mzee Mashaka Gambo kwa kufiwa na mkewe ambaye pia ni mama mzazi wa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo kwa kufiwa na mama yake mzazi Marehemu Rehema Paul Mumbuli  leo Aprili 18 mwaka huu. (Picha na Ikulu)

No comments: