Thursday, April 12, 2018

WATU 17 WAPOTEZA MAISHA WENGINE 14 WAJERUHIWA VIBAYA


KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida wameripotiwa watu 17 kufariki dunia na wengine 14 kujeruhiwa vibaya, katika ajali ya basi iliyotokea kwa makosa ya kibinadamu baada ya dereva wa gari hilo kupoteza muelekeo.

Imefafanuliwa kuwa hali hiyo ilitokana na dereva huyo akijaribu kulikwepa Lori lililokuwa likijielekeza katika upande wake.

Mkuu wa Wilaya ya Narok nchini Kenya, George Natembeya alisema kuwa basi hilo lilikuwa na abiria 63.


Miongoni mwa watu waliopoteza maisha kwenye ajali hiyo, walikuwemo pia watoto watatu.

No comments: