Na Muhidin Amri,
Madaba.
BAADHI ya Wakulima wanaozalisha zao
la tangawizi katika kijiji cha Magingo na Mkongotema, kata ya Mkongotema
Halmashauri ya Wilaya ya Madaba Mkoani Ruvuma wameiomba Serikali kuwatafutia
soko la kuuza zao hilo ili kuweza kukomesha vitendo vya walanguzi wanaokwenda
kuwalaghai wakulima hao kununua tangawizi kwa bei ndogo.
Hali hiyo imefuatia kuporomoka kwa bei
ya zao hilo katika jimbo la Madaba kutoka shilingi 4,000 mwaka 2015/2016 hadi
kufikia shilingi 700 mwaka 2017 hivyo kuwafanya wakulima hao kuvunjika moyo wa
kuendeleza kuzalisha.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti na
waandishi wa habari waliotembelea wakulima hao ili kujionea changamoto hiyo
walisema kuwa wakati umefika sasa kwa Serikali kutambua matatizo ya wakulima wa
zao la tangawizi na kuyatafuta ufumbuzi wa haraka.