Thursday, December 18, 2014

AFARIKI DUNIA BAADA YA KUKANYAGWA NA LORI



Na Steven Augustino,
Tunduru.

KIJANA mwenye umri wa miaka 15 aliyefahamika  kwa jina la Khasim Mohammed, mkazi wa kijiji cha Mtangashari wilayani Tunduru mkoa wa Ruvuma amefariki dunia baada ya kupata ajali katika gari, ambalo alikuwa ameomba msaada ili aweze kusafiri.

Mihayo Msikhela kamanda wa polisi wa mkoa huo, alisema kuwa marahemu huyo alifariki dunia papo hapo baada ya kuanguka katika gari hilo.

Alisema ajali hiyo ilitokana na gari lenye namba za usajiri T699 BCX mali ya kampuni ya China Civil Engineering Construction Co.Ltd (CCECC) inayojenga kipande cha barabara kilometa 58.7 kutoka Tunduru mjini hadi Matemanga. 


Alisema baada kijana huyo kulisimamisha gari hilo dereva wa lori hilo aina ya SEYA 33G ambalo ni maalum kwa ajili ya kubebea kifusi, alisimama na kufanya makubaliano ya kumchukua hadi Tunduru mjini.

Alifafanua kuwa lori hilo lilikuwa likiendeshwa na dereva Fredy Chasua, ambapo ghafla aliliondoa gari hilo wakati kijana huyo akiwa anaendelea kupanda hali ambayo ilimfanya ateleze na kuanguka chini, na kukanywagwa na magurudumu ya nyuma na kusababisha kifo chake papo hapo.

Kamanda Msikhela aliendelea kufafanua kuwa baada ya tukio hilo, dereva huyo alikimbia na kutokomea kusiko julikana, na kwamba Polisi wanaendelea kumsaka ili sheria iweze kufuata mkondo wake.

No comments: