Monday, February 27, 2017

MAGHEMBE ASHANGAZWA NA UTAJIRI WA VIVUTIO VYA UTALII ZIWA NYASA

Wageni mbalimbali wakiwa katika eneo la viwanja vya Makumbusho ya Taifa ya Vita vya Majimaji mjini Songea mkoani Ruvuma.
Na Kassian Nyandindi,   
Songea.

WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe ameshangazwa na utajiri wa vivutio vya utalii vilivyopo katika mkoa wa Ruvuma, wakiwemo aina ya samaki wa mapambo zaidi ya 400 katika ziwa Nyasa mkoani humo na viumbe wengine adimu waliopo katika ziwa hilo.

Kwa ujumla viumbe hao licha ya kuwa ni adimu pia wamekuwa hawapatikani sehemu yoyote ile hapa duniani.

Profesa Maghembe alishangazwa na hayo wakati alipokuwa akizungumza katika sherehe za kumbukizi ya miaka 110 ya Vita vya Majimaji, zilizofanyika kwenye viwanja vya Makumbusho ya Taifa ya Majimaji Songea mkoani hapa.

Alisisitiza kuwa ni fursa pekee sasa, kuendelea kutangaza vivutio hivyo ili viweze kuleta tija kwa Taifa hili kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho wakiwemo Wananyasa na mkoa wa Ruvuma kwa ujumla.



Kwa ujumla ziwa Nyasa lipo katika wilaya ya Nyasa mkoani humo ambapo licha ya kuwepo kwa samaki hao pia kumekuwa na vivutio vingi vya utalii kama vile visiwa vya kuvutia vilivyopo kwenye ziwa hilo, milima na mawe mazuri ya kuvutia ambayo yana historia nzuri za kale kwa watu wanaokwenda kutembelea huko kujifunza mambo mbalimbali.









No comments: