Sunday, October 8, 2017

MATUKIO KATIKA PICHA SIKU YA MAHAFALI DARASA LA SABA DE PAUL SONGEA

Mgeni rasmi katika mahafali ya wanafunzi wa darasa la saba shule ya De Paul Msamala Manispaa ya Songea Kamishina wa elimu Tanzania, Dokta Edicome Shirima akiangalia vifaa vya masomo ya sayansi kwa wahitimu wa darasa la saba wa shule hiyo.

Wahitimu wa darasa la saba shule ya De Paul Msamala wakionesha umahili wao wa kucheza muziki wakati wa mahafali yao ya kumaliza elimu ya msingi shuleni hapo.

Kamishina wa elimu Tanzania Dokta Edicome Shirima akimzawadia mwanafunzi Amri Mmanja ambaye alifanya vizuri katika michezo na taaluma wakati wa mahafali yao ya kuhitimu darasa la saba katika shule ya De Paul Msamala iliyopo Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma.

Mama mzazi wa Amri Mmanja Farida Komba, akimpatia zawadi mtoto wake Amri Mmanja baada ya kuhitimu elimu ya msingi wakati wa mahafali yake ya darasa la saba iliyofanyika juzi katika shule ya De Paul iliyopo Msamala katika Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma.

No comments: