Saturday, January 12, 2013

AFARIKI DUNIA KUTOKANA NA KUGONGANA NA GARI USO KWA USO

Na Steven Augustino, 
Songea.
 
Mwendesha Pikipiki mkazi wa kijiji cha Lipokela Songea vijijini Issack Gillas(31) amefariki dunia katika ajali mbaya ya kugongana  Pikipiki aliyokuwa akiiendesha na gari lililokuwa likipita barabarani.
Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Ruvuma Deusdedith Nsemeki alisema, tukio hilo lilitokea Januari 8 mwaka huu katika Barabara ya Songea kwenda Mbinga mkoani humo.
Nsemeki alisema kuwa katika tukio hilo pikipiki hiyo yenye namba za usajiri T. 937 CCA  iligongana uso kwa uso na gari aina ya Toyota Hilux lenye namba za usajili T. 730 AXZ.
Alifafanua kuwa chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi aliokuwa akiendesha dereva wa gari hilo, ambaye alidai kuwa hadi sasa hajafahamika jina lake kutokana na kukimbia na kulitelekeza gari hilo katika eneo la tukio hilo.
Alisema kwamba kufutia hali hiyo gari hilo limehifadhiwa katika kituo kikuu cha Polisi, kilichopo katika manispaa ya Songea huku jeshi hilo likiendelea na uchunguzi zaidi.
Akizingumzia tukio hilo mganga mfawidhi wa  wa hospitali ya koa wa Ruvuma(HOMSO) Dkt. Anton Ngaiza alisema, kuwa chanzo cha kifo hicho kilisababishwa na marehemu kutokwa damu nyingi.
Alisema marehemu aliumia vibaya kichwani pamoja na sehemu za kifua, kuliko sababishwa na kugongwa vibaya na gari hilo.

No comments: