Thursday, January 17, 2013

MATUMIZI YA DAWA ZA ASILI KATIKA SHAMBA LA KAHAWA NI JAMBO AMBALO HALINA MJADALA

Mkulima Manfred  Komba wa kikundi cha Unango akipulizia dawa ya asili shambani kwake kwa lengo la kuua wadudu waharibifu wa zao la kahawa. Kwa mujibu wa maelezo ya wataalamu wanasema kuwa hata mkojo wa Ng'ombe umekuwa ukitumika katika kazi ya kuua wadudu ambapo unavundikwa kwa siku 14 katika chombo maalum, baada ya hapo unachanganywa na majivu na kisha kupulizwa kwa siku saba katika mmea wa kahawa. Ni dawa nzuri ambayo inaua wadudu aina ya Vidung'ata na Vidugamba wakulima wanashauriwa sana kutumia njia hiyo na kuepukana na madawa ya viwandani ambayo yana kemikali kali ambazo hupoteza ladha ya tunda kahawa.

No comments: