Thursday, May 23, 2013

BREAKING NEWS: SHEHA ZANZIBAR AMWAGIWA TINDIKALI

Sheha wa Tumondo, aliyemwagiwa Tindikali.

















 
ZANZIBR:

Mohamed Omary Said, amemwagiwa tindikali na mtu asiyejulikana na hivyo kupata maumivu makali sehemu yake ya kifua na jicho kuumia vibaya.

Sheha huyo alikimbizwa katika hospitali ya Mnazi mmoja, mjini Unguja ambako anatiwa matibabu ya dharura.


Kamanda wa polisi wa mkoa wa mjini Magharibi, Mukhadam Khamis, alisema chombo kilichotumika kumwagia tindikali Sheha huyo kilipatikana eneo la tukio na kwamba polisi, imekichukua kwa kukichunguza kitaalam ili kugundua aliyekuwa akikitumia kwa kuangalia alama za vidole.


Sheha huyo alimwagiwa tindikali jana usiku wakati alipotoka nje ya nyumba yake kuchota maji na ndipo mhalifu huyo alipomwagia tindikali na kwamba hakuweza kumtambua. (Kwa hisani ya www.habarimasai.com)



No comments: