Friday, May 31, 2013

CUF NA CHADEMA WATII AMRI YA KUOMBA RADHI BUNGENI

 


    Mbunge wa Jimbo la Nyamagana, Ezekiel Wenje.


















    Dodoma, 
    Tanzania. 

    Chama cha CUF na Chadema hivi punde Bungeni , vimekubali kuomba radhi kutokana na vurugu zilizosababishwa na CUF  yenye mrengo wa Kiliberali  na Chadema imemfanya hivyo kutokana na kuihusisha CUF na masuala ya ushoga na usagaji.

    Vyama hivyo vimeomba radhi baada ya Kamati ya Maadili ya Bunge kufanya kikao  kuanzia saa 11:00 jioni mpaka saa 2:30 usiku na kukubaliana kila chama kumuomba spika radhi, na pia kuliomba Bunge radhi kutokana na vurugu za jana.

    CUF wamelazimika kumuomba spika radhi; kuomba radhi Bunge na kuwaomba radhi Chadema kwa kumtukana Waziri kivuli wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Ezekeil Wenje wakati akisoma hutuba yake ambayo ndani yake ilieleza sera za mrengo wa Kiliberali ambazo  pamoja na mambo mengine ni ushoga na usagaji.  


    Awali Mnadhimu wa Chama cha CUF Rashid, wakati akiomba radhi aliipongeza Kamati ya Maadili na Chadema kwa kufikia muafaka kwa maslahi ya Taifa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

    “ Napenda kuomba radhi kwa watu wote walioumizwa na vurugu za jana,” alisema Rashidi.

     Naye Kiongozi wa Kambi rasni ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe alisimama Bungeni na kuwaomba radhi CUF, Bunge na Spika kutokana na hotuba ya jana iliyosomwa bungeni jana na Wenje.

    Awali kabla ya kuomba radhi leo, Freeman Mbowe jana kwenye kikao cha Kamati ya Maadili ya Bunge, alisema kwamba CUF wanafuata mrengo wa Kiliberali ambao msingi wa sera zao ni shoga na usagaji na kwamba hawakufanya kos.

    Pia alisema CUF alimdhalilisha Wenje (Chadema), CUF walichana hotuba yao na kuwaudhi na kuwakera Chadema.

    Kutokana na hali hiyo CUF walishauriwa kuomba radhi jambo ambalo wametii amri hiyo leo asubuhi.

    Wakati akisoma taarifa ya kamati hiyo  John Chiligati ambaye ni Mbunge wa jimbo la Manyoni mashariki alisema jana CUF walikiri kwenye kamati hiyo kwamba wao ni wanachama wa mrengo wa Kiliberali, lakini chama chao hakikubaliani na sera zote kama za ushoga na usagaji kwa kuwa serikali imeshatoa msimamo kwamba haiungi mkono mambo hayo.

    No comments: