Monday, May 27, 2013

DOKTA SLAA ASEMA VURUGU ZA MTWARA ZINASABABISHWA NA UMASKINI, HUKU AKIKINYOSHEA KIDOLEA CHAMA CHA MAPINDUZI

Dkt. Willbroad Slaa.


  












Editruda Mashimi,
Dar es Salaam.

WAKATI Serikali ikiendelea kuwatupia wanasiasa lawama kuhusiana na vurugu za wakazi wa Mtwara, wanaopinga hatua ya Rais Kikwete na serikali yake kusafirisha gesi hadi jijini Dar es Salaam kwa njia ya mabomba, Katibu mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Dkt. Willbroad Slaa, amesema kwamba machafuko yanayotokea katika mkoa huo hayasababishwi na mambo ya kisiasa, isipokuwa ni umaskini unaoikabili nchi.

Dkt. Slaa alisema kwamba umaskini huo unaosababisha vurugu za Mtwara unachangiwa na CCM tangu zama za kale na si kwa siasa za sasa. 

“Yanayotokea Mtwara ni matokeo ya umaskini ambao CCM imewaletea wananchi,

“Mtwara wanakumbuka ya Mwadui, Geita na North Mara sasa wanayakataa”, alisema Dkt. Slaa katika ukurasa wake wa Tweeter.


Alisema kwamba wananchi hao  wameamua kufanya yote hayo kwa kuangalia wenzao wa mikoa mingine iliyojaliwa kuwa na mali nyingi katika mikoa yao, na bado hawanufaiki matokeo yake inakuwa ni mali yakuwanufaisha wengine bila wao kupata faida yoyote ile.

Katika hatua nyingine Dkt. Slaa alisema kwamba serikali isikimbilie kulaumu wanasiasa, bali itambue kwamba siasa chafu zinafanya kazi kama watu ni maskini, lakini kama nchi itakuwa tajiri siasa chafu haziwezi kuwepo.

No comments: