Friday, May 31, 2013

MATOKEO KIDATO CHA NNE 2012 YATANGAZWA UPYA, BAJETI YA KAWAMBWA YAUNDIWA ZENGWE


 
Waziri wa Elimu na Mfunzo ya Ufundi, Dkt. Shukuru Kawambwa. 



















Dar es Salam,
Tanzania.


WAKATI Baraza la Mitihani Taifa (NECTA) likitangaza matokeo mapya ya kidato cha nne, baada ya kufanya marekebisho ya alama za viwango vya ufaulu, njama za kukwamisha hotuba ya Bajeti ya Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dkt. Shukuru Kawambwa zinaandaliwa.


Habari zilizonaswa kwa msaada wa vyanzo mbalimbali  vinaeleza kuwa, Wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wamejipanga kukwamisha hotuba ya Wizara hiyo, kwa madai kwamba Waziri huyo ameshindwa kusimamia sekta ya Elimu.

Vyanzo hivyo vinadai kwamba, Wabunge wamepania kukwamisha hotuba hiyo na kumtaka Waziri huyo ajiuzuru ili kukisafisha chama hicho kutokana na aibu ya mkanganyiko wa kufeli kwa wanafunzi mwaka huu.

"Hotuba ya Wizara ya Eilimu haiwezi kupitishwa kirahisi kama Kawambwa hata jiuzuru, hatuwezi kuendelea kuwa na mawaziri wanaoshindwa kuwajibika ipasavyo katika setka zao, kitendo cha mawaziri hao kushindwa kuwajibika ipasavyo ndiyo kunachangia kuharibu Chama", kilisema chanzo hicho.

"Huu mpango unaendelea kusukwa na wabunge wa CCM waliopania kurudisha heshima ya chama, lazima tuanzie ndani kuwajibishana wenyewe kabla ya wapinzani kuanza, kwani tukishindwa sisi watatumia udhaifu wetu kuwashawishi wananchi, na hatimaye watazidi kuichukia Serikali", kiliendelea kufafanua. 

Wakati Waziri Kawambwa akiandaliwa zengwe la kung'olewa, NECTA imetangaza matokeo yaliyoongeza kiwango  cha  ufaulu kufikia asilimia kati ya 54 na 57 wiki hii, pamoja na yale ya kidato cha sita ambayo pia yamechelewa kutangazwa.
 

 

 

No comments: