Friday, May 31, 2013

MATOKEO KIDATO CHA SITA, ASILIMIA 93 WAFANYA VIZURI, 89 MATOKEO YAZUILIWA

  Na Mashirika mbalimbali ya Habari,

BARAZA la mitihani hivi sasa limetangaza matokeo ya kidato cha sita mwaka 2013. Matokeo hayo yatapatikana muda mfupi ujao kwenye tovuti yao.

Asilimia 93 ya waliofanya mtihani huo wa kidato cha 6 wamefaulu.

Shule ya kwanza iliyoongoza ni Marian Girls ya mkoani Pwani na ya pili ni Mzumbe ya Morogoro.


Mwanafunzi wa kwanza wa kiume kwa masomo ya sayansi ni Erasmi Inyase kutoka Ilboru, na kwa wasichana ni Lucy Light wa Marian girls.

Upande wa masomo ya Biashara mwanafunzi wa kwanza ametoka shule ya Tusiime anaitwa Erick Robert.

Wanafunzi 89 matokeo yao yamezuiliwa kwa sababu mbalimbali.

Wanafunzi watakaothibitika kuwa walikuwa na matatizo ya kiafya, watapewa nafasi ya kurudia mtihani.

No comments: